Baada ya migogoro mingi inayoikumba kundi la Bongo
Movie na kusababisha baadhi ya wasanii wanaounda kundi hilo kulikimbia
huku chanzo kikubwa kikidaiwa ni umbea, majungu na kutoaminiana kati ya
wanakikundi. Jana kupitia akaunti yake ya Instagram Frola Mvungi ambae
pia ni mke wa msanii H Baba ametangaza rasmi kujitoa katika Kundi hilo,
huku sababu zikiwa ni kama za wenzake waliojitoa.
Hiki ndo alichokiandika katika post yake ya Instagram ” Dah..kutokana
na mambo yanayoendelea bongo movie club ambayo Kiukweli hayaninufaishi
chochote. Zaidi ya kuniongezea chuki kwa watu Bila sababu,Imekuwa ni
tatizo kuwa upande wowote Bila malumbano,upendooo,fitna na roho mbaya
zinazotengenezwa na sisi wasanii ndani ya club zilinifanya niondoke.
Mara ya Kwanza but.! @stevenyerere2 alinishawishi Baada ya kuwa kiongozi
nikiona mabadiliko nikarudi ila sasa.! stevenyerere ameng’atuka.
Kwasababu ya kutetea wanyonge dah!waliobaki. Ndo wale walionifanya
niondoke mwanzo..MAAMUZI magumu sina budi kusema kuwa ni bora nikae
mwenyewe nifanye kazi zangu Bila problem Bila kufitinishwa na mtu
yeyote..wale ni wasanii wenzangu nawapenda but sera za pale
zimenishinda..natangaza. Kujitoa leo Rasmi siwezi migogoro ya Kila siku”
Post a Comment