MWanamke mwenye umri wa miaka 40 amebakwa akiwa anamtembeza Mbwa wake katika mtaa wa Salford nchini Uingereza.
Alikuwa
anatembea karibu na jumba la New Bank Towers siku ya Jumapili
alipokutana na mwanamume mmoja ambaye hakumfahamu ila wlaitembea pamoja.
Walipowasili naye katika barabara ya Mount, alisukumwa kichakani na kubakwa na mwanamume huyo.
Inaarifiwa
mwanamume huyo anayesakwa na polisi, alimhadaa mwanamke huyo na kisha
kumsukuma kichakani kabla ya kumtendea uovu huo.
Maafisa wa polisi, wanasema kuwa kitendo hicho kilikuwa kibaya sana na kwamba wanafanya uchunguzi.
Post a Comment