Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi akitoa ufafanuzi
kuhusu makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa kati ya viongozi
wa Bunge maalumu la katiba watakao kabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Kikwete na wa Zanzibar Dkt Mohamed
Sheni kwa waandishi wa habari, makabidhiano hayo yatafanyika Oktoba 08,
2014 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.(Picha na John Banda wa
Pamoja Blog)
Waandishi
wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Dkt, Rehema Nchimbi kwa makini wakati alipokua akielezea kuhusu
makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa keshokutwa Oktoba, 08
mwaka huu katika uwanja wa jamhuri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete na Dkt Mohamed Sheni ndiyo watakabidhiwa.
WANANCHI
wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani wametakiwa kufika katika uwanja wa
jamhuri mjini Dodoma jumatano ya oktoba 8, 2014 kwa ajili ya
kushuhudia tukio la kihistoria kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa na
bunge maalumu la katiba.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi wakati
akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema Tukio hilo
litafanyika hapa mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri kuanzia saa
6:00 Mchana na Milango ya uwanja wa Jamhuri itafunguliwa kuanzia saa
12:00 asubuhi.
Mkuu
huyo wa Mkoa amesema watu watakaojitokeza ili kushuhudia tukio hilo
watakuwa wengi hivyo kwa kuzingatia kuwa milango ya uwanja wa Jamhuri
itafunguliwa mapema, wananchi wanashauriwa kuwahi kufika viwanja vya
Jamhuri na kuhakikisha kuwa kila mtu atakayehudhuria awe tayari amekaa
kwenye nafasi yake ifikapo saa 5:00 asubuhi.Dkt
Nchimbi amesema tukio hilo litahudhuriwa na Marais wastaafu wa
Tanzania, Marais wastaafu Zanzibar, Viongozi wa kitaifa na watendaji
wakuu, Viongozi wakuu wastaafu, Maspika wastaafu, Waheshimiwa Mabalozi
na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa, Taasisi za Kidini, Taasisi
zisizo za kiserikali na wamiliki wakuu wa vyombo vya habari.
Amesema
Vilevile kutakuwepo na Makundi mbalimbali kutoka mikoa ya Tanzania bara
na Zanzibar. Makundi hayo ni pamoja na Wafugaji, Wakulima, Wavuvi,
Wanawake, Vijana, Wazee, Wachimbaji madini wadogo, Walemavu na Wasanii.
Aidha
Dkt, Nchimbi ameseama Tukio hilo la Kihistoria litatanguliwa na tukio
muhimu na maalum la kuomba Dua na Shukrani kwa kukamilika salama kwa
shughuli za “Bunge Maalum la Katiba” hapa Mkoani Dodoma tofauti na nchi
nyingine katika viwanja vya Nyerere Squere hapo kesho saa 10 jioni.
Post a Comment