Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru.
Mmoja
wa mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema
ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani
-Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka
Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.
Aliongeza
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la
abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso
kwa uso na lori hilo.
Post a Comment