Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiangalia ramani ya
Tanzania inayoonyesha mchoro wa reli ya Kati inayotarajiwa kujengwa
upya na kwa viwango vya kisasa wakati alipokutana na uongozi wa juu wa
makampuni ya China yakiongozwa na China Railway Group Ltd. Makampuni
mengine ni SINOSURE, Exim Bank, China Development Bank na China
Agriculture Development Bank. Rais Dkt. Kikwete yuko nchini China kwa
ziara rasmi ya kikazi (State Visit).
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya
China Railway Group Limited Bwana Li Changjin na msafara wake kuhusu
mpango wa serikali ya Tanzania wa kujenga reli mpya na ya viwango vya
kisasa kutoka Dar Es Salaam hadi Kigoma, Tabora kwenda Mwanza, Kaliua
kwenda Mpanda hadi Ziwa Tanganyika. Mazungumzo hayo yalifanyika huko
Beijing tarehe 24.10.2014.John Lukuwi
Post a Comment