KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14), mkazi wa
Chanika nje kidogo ya jiji la Dar es Slaam amelalamikia umeme kubadili
sura yake baada ya kuungua vibaya na moto uliosabishwa na hitilafu ya
nishati hiyo katika nyumba yao iliyotokea wiki mbili zilizopita.
Kijana anayefahamika kwa jina la Saadam Hussein (14) aliyeungua
vibaya kutokana na hitilafu ya umeme.Akizungumza na gazeti hili katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi namba 23 iliyopo katika jengo la
Sewahaji, baba wa kijana huyo Hussein Ally alisema mtoto wake anayelala
katika chumba karibu na dukani, alisikia vitu vikidondoka, lakini
alipojaribu kuamka, akakutana na moto huo ukiwa umekolea.
Alisema kijana wake alitaka kuokoa mali zilizokuwa zinateketea na
moto, lakini moshi na ukali wa moto ulimzidi nguvu na kusabisha
kushindwa kuona na hivyo kuungua huku duka lote likiteketea.Alisema
pamoja na mali zote zilizokuwepo dukani kuteketea, lakini pia mauzo ya
siku 9 yanayokadiriwa kufikia shilingi milioni 1.9 nayo yaliungua.
“Kijana wangu ameungua vibaya sana, hapa ninamuomba Mungu tu maana hata
kuongea ni shida,” alisema baba huyo kwa huzuni.Muuguzi aliyekuwa zamu,
ambaye alikataa kutaja jina lake kwa vile siyo msemaji wa hospitali
hiyo, alisema kijana huyo ameungua vibaya, ingawa bado hawajajua ni kwa
asilimia ngapi
Saadam
Hussein akiwa na Baba yake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.“Kuna
viwango cha kuungua, siwezi kujua ameungua kwa asilimia ngapi lakini
sehemu kubwa ya mwili wake umeuungua vibaya,” alisema.
Baba wa mtoto huyo alisema kijana wake alikuwa akifanya biashara hiyo
kwa lengo la kuanza elimu ya sekondari ya binafsi na kutokana na
kuungua kwa duka hilo, amebaki hajui la kufanya, wkani hata gharama za
matibabu hospitalini hapo zinamtesa.
Aliwaomba watu wote walioguswa na kuungua kwa mwanaye kumsaidia kwa
kutumia namba zake za simu ambazo ni 0786 89 51 14 au 0754 67 62 39.
Post a Comment