Katibu Mkuu wa CCM,
Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa uwanja wa ndege mjini Dodoma mapema leo
asubuhi na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo, Mh. Adam Kimbisa,tayari kwa kuanza
ziara ya siku tisa, yenye lengo la kukagua, kuhimiza miradi ya maendeleo ya
wananchi pamoja na kuangalia uhai wa chama, ambapo mara baada ya
kuwasili amefanya
mkutano wa ndani na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Mpwapwa yenye
majimbo mawili ya Uchaguzi.Kinana ametokea Mkoani Ruvuma mara baada ya kushiriki
mazishi ya aliekuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi,Marehemu Kapteni John
Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa,Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa
Dodoma Mh.Chiku Galawa mapema leo asubuhi mara baada ya kuwasili uwanja wa
ndege,tayari kwa kuanza ziara ya siku 9 mkoani humo,
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa,Mh.Addam Kimbisa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na
Ujumbe wake pamoja na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili
katika ofisi za CCM Wilaya ya Mpwapa mapema leo asubuhi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na baadhi ya Wanachama wa CCM waliofika
mapema leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mpwapwa kumpokea Ndugu Kinana na Ujumbe
wake,ambapo anaanza rasmi ziara yake wilayani humu na vitongoji
vyake.
PICHA
NA MICHUZIJR-MPWAPWA.
Post a Comment