Mwanamuziki wa miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amepondwa vibaya katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mhe. Kapt. John Komba, baada ya kuvaa kigauni kilichombana na kumuonyesha maungo yake ya mwili mbele ya viongozi mbalimbali wa Serikali akiwepo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Mwanamuziki wa
miondoko ya mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba pamoja na wasanii wenzake
kwenye msiba wa Komba.
Baadhi ya watu waliofika katika Viwanja vya Karimjee
vilivyopo Posta jijini Dar, walianza kunong’onezana baada ya mwanamuziki huyo
kujitokeza mbele na kuimba kipande cha shairi lake huku wakisema kuhusu kigauni
alichovaa bi’dada huyo.
“ Jamani hii aliyovaa si ‘tight’ kabisa, maana yupo
tofauti na wenzake ambao wote wamevaa nguo za heshima zinazowasitiri maumbo
yao, kwa nini yeye ameamua kuvaa hivyo?” alisikika mama mmoja ambaye naye
alikuwemo kwenye maombolezo.
Mwandishi wetu alimtafuta Shilole na kumuuliza
kuhusiana na hilo alisema hakuvaa vibaya isipokuwa alionekana vile kutokana na
umbo la mwili wake.
Mpekuzi blog
Post a Comment