Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima alisema hayo mjini Dar es Salaam wakati alipokuwa akifungua kikao cha
Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA).
Alisema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete itaendelea
kusaidia NIDA ili kufikia malengo ya serikali ya Awamu ya Nne ya kila Mtanzania
kuwa amesajiliwa na kupata kitambulisho chake.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa, Dickson Maimu, alisema mpaka sasa NIDA imepiga hatua
kubwa katika suala la Usajili na Utambuzi wa watu na ugawaji wa vitambulisho vya
taifa.
Mpaka sasa NIDA imefanikiwa kusajili wananchi milioni
6.1, ambapo kati ya hao, wananchi milioni 2.8 tayari wameshakamilisha hatua za
usajili kwa maana ya kuchukuliwa alama za kibayolojia kwa Zanzibar na Bara.
Jumla ya vitambulisho milioni 1.7 vimezalishwa na kugawanywa kwa
wananchi.
NIDA tayari imekamilisha usajili wa awali Tanzania
Zanzibar, mkoa wa Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro na
Tanga.
Akielezea changamoto kubwa ya sasa inayoikabili Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa, Maimu alieleza changamoto kubwa kuwa ni rasilimali
fedha na rasilimali watu na hivyo kuzorotesha utendaji na mikakati ya kuendelea
na Usajili katika mikoa ya Tanzania.
"Mipango wa sasa ni kuanza rasmi kwa matumizi ya
vitambulisho vya taifa, na tayari vikao na wadau wanufaika vimeshafanyika kwa
Bara na Visiwani na muda si mrefu Vitambulisho vitaanza kutumika kama nyaraka
rasmi ya utambulisho," alisema.
Akizungumza na wafanyakazi hao, Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Pereira ameahidi serikali kupitia Wizara yake kuendelea
kuongezea nguvu Mamlaka kufikia malengo iliyojiwekea.
Post a Comment