Watu 35
wamefariki dunia na wengine 55 wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na
nyumba zao kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali
iliyonyesha usiku wa kuamkia leo, kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Mbuzi
wakiwa wamepoteza maisha baada ya kupigwa na mvua ya mawe.WATU 38
wamefariki Dunia huku wengine zaidi ya 60 wakijeruhiwa vibaya baada ya
mvua kubwa ya mawe iliyoambatana upepo mkali kunyesha katika kijiji
cha Mwakata kata ya Isaka Wilayani Kahama Mkoani shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema kuwa
tukio hilo lilitokea usiku wa march tatu majira ya saa tatu za usiku na
kusababisha maafa hayo ambayo hayajawahi kutoka katika Mkoa wa
Shinyanga.
Kamugisha katika maafa hayo watu 35 walifariki papo hapo huku
majeruhi zaidi ya 60 wakikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama
kwa ajili ya kupatiwa matibabu na jitihada zaidi za uokozi zikiendelea
katika kijiji hicho
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Joseph
Ngowi akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa amepokea majeruhi
zaidi ya 60 na kati yao watatu wamefari wakati wakiendelea na matibabu
katika Hospitali hiyo.
“Hatuna idadi kamili ya watu waliojeruhiwa au waliokufa na tumetuma
madaktari wetu kwenda katika kijiji hicho kwa ajili ya huduma ya kwanza
pamoja na kufanya uchunguzi ili kubaini idadi kamili ya waliofariki
Dunia”, Alisema Joseph Ngowi.
Dr, Ngowi alisema kuwa kutokana na umbali uliopo kutoka katika eneo
la tukio hadi katika Hospitali ya Wilaya wamelazimika kutuma jopo la
madaktari kwenda kwenye eneo la tukio ili kubaini waliofariki na
kuhidhinishwa kwa maziko ili kupunguza gharama kwa wananchi waliofiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya alisema Kamati
ya ulinzi na usalama ya Wilaya inategemea kukaa mchana huu kwa ajili ya
kutathimini takwimu za uharibifu wa mali pamoja na idadi ya nyumba
zilizokumbwa na maafa hayo.
Alisema kuwa Jeshi la zima moto kwa kushirikiana na Wananchi
wanaendelea na shughuli za uokoaji na huenda idadi ya waliokufa pamoja
na majeruhi ikaongezeka katika tukio hilo.
Hata hivyo Majeruhi waliolazwa katika Hspitali ya Wilaya ya Kahama
wakizungumzia kuhusu tukio hilo walisema kuwa Mvua hiyo ilionyesha kwa
upepo mkali ulioambatana na mawe makubwa hali iliyosababisha
uliosababisha nyumba kuezuliwa pamoja na kung’olewa kwa miti.
“Tulikuwa tumelala majira ya saa tatu usiku ghafla tulisikia upepo
mkali ukiambatana na mvua kubwa ya mawe na maji mengi kuingia ndani na
ghafla nyumba yangu ilianguka na kupoteza wajukuu wangu wanne,” alisema
Paulina Malongo mmoja wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali hiyo
Post a Comment