Kumekuwa
na taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya kijamii kuhusu hali ya
Afya ya Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Ofisi ya Bunge inapenda
kuutangazia umma na Wananchi wote kuwa, taarifa hizo zinazosambazwa
katika baadhi ya Mitandao si za kweli, bali ni uzushi mtupu.Ukweli
ni kwamba Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ni Mzima wa afya na
hivi sasa yuko jimboni kwake Kongwa, Mkoani Dodoma akifanya maandalizi
ya Mwisho ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana
itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii na hasa Jimboni Kongwa, Dodoma.Ofisi
ya Bunge inapenda kuwatoa hofu Wananchi wote na kuwataka kuzipuuza
taarifa hizo kwa kuwa si za kweli bali ni uvumi unaonezwa na watu
wachache wenye nia ovu ya kujenga hofu miongozni mwa Wananchi kupitia
mitandao ya kijamii.
Aidha
tunapenda kutoa rai kwa watu wote kuacha kusambaza taarifa hizo potofu
na badala yake kama kuna taarifa zozote kuhusu Ofisi ya Bunge au
Viongozi wake wafanye jitihada za kuthibitisha taarifa hizo kwenye
Mamlaka husika kabla za kuzisambaza.
Ofisi
ya Bunge inao utaratibu rasmi wa kutoa taarifa muhimu kwa wananchi na
umma kwa ujumla, hivyo si vyema kwa watu kusambaza taarifa potofu kuhusu
Bunge na viongozi wake ambazo zinaweza kuleta usumbufu miongoni mwa
Viongozi na baadhi ya wananchi.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
4 MACHI 2015
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge
DAR ES SALAAM
4 MACHI 2015
Post a Comment