Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya
Mpwapwa kwenye uwanja wa mikutano Mnarani ambapo aliwaambia wananchi hao
kuwa ahadi zilizoahidiwa na CCM zitatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi wa
Mpwapwa mjini na kuwaambia katika uongozi wake atawapa nafasi wale watu
wanaotakiwa na wananchi wenyewe kuwaongoza na kusema hakutokuwa na
makosa ya kukata majina.
Umati wa
Watu uliohudhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
ambaye ameanza ziara ya mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukagua na
kufuatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kujenga na kuimarisha
chama mkoani humo.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mpwapwa mkoani
Dodoma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mnarani.
Mkazi wa
kata ya Lupeta wilayani Mpwapwa Gloria Manihuzi akiwakilisha kilio chao
cha muda mrefu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (hayumo
pichani) cha matatizo ya mawasiliano katika kijiji chao na kusisitiza
kunahitajika juhudi za haraka zifanyike wapate mnara wa simu.
Mwalimu
Mstaafu Silvanus Hosea akitoa maoni yake wakati wa mkutano wa hadhara
kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alisema viongozi
wa CCM hasa wanaogombea nafasi za uongozi wasipende kutoa ahadi
zisizotekelezeka kwani zinachangia kupoteza imani ya wananchi kwa chama.
Mkulima
Bora wa mwaka 2014 Anna Mlewa akimuonesha Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman
Kinana shamaba lake lililopo Belege la mazao ya karanga na mahindi
ambapo Anna ni mmoja wa wakulima wa mfano wanaotumia kanuni bora za
kilimo,kulia ni mume wa Anna,Ruben Mlewa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la
karanga la Bi. Anna Mlewa, wengine ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa
Chiku Galawa (kulia).
Diwani wa
Belege Damas Nang'unda akizungumzia maendeleo na changamoto wapatazo
wananchi wake wakati wa mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana aliyepita kuwasalimia wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mzee Robert Matonya mkazi wakijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubiawakazi wa Kisokwe kabla ya kushiriki ujenzi wa Zahanati.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea tofali kutoka kwa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa wakati wa
kushiriki ujenzi ya zahanati ya Kisokwe.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa akishiriki ujenzi wa zahanati ya Kisokwe .
Bweni lililoungua moto la shule ya sekondari Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi lililoungua moto mapema mwanzoni mwa mwaka. Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mpwapwa wakifurahia kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kutembelea bweni la wanafunzi lililoungua moto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya CCM tawi la Mpwapwa mjini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akiwahutubia wananchi wa
Mpwapwa mkoani Dodoma na kuwaambi wawe makini na baadhi ya vyama vya
siasa vinavyo andaa vijana kuingia msituni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi lililoungua moto mapema mwanzoni mwa mwaka. Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mpwapwa wakifurahia kusalimiana na Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kutembelea bweni la wanafunzi lililoungua moto.
Post a Comment