Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MARAFIKI WA LOWASSA WAFUNIKA ARUSHA

SAM_2786
 
SAM_2861
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta  akicheza sambamba na Mkurugenzi wa kituo cha Radio 5 Robart Francis staili ya shikorobo juzi kwenye party ya usiku wa marafiki wa Lowassa ulifanyika katika ukumbi wa triple A jijini Arusha.
SAM_2786Kundi la marafiki  wa Lowasaa chini ya umoja wao unaojulikana kama “4 U Movement”wakishangilia katika party hiyo
SAM_2840Katibu mwenezi wa CCM mkoani Arusha, Isack Joseph  maarufu kama "kadogoo"akicheza na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta katika party ya usiku wa marafiki wa Lowassa uliofanyika katika ukumbi wa Triple A jijijni Arusha nakuhudhuriwa na watu mbalimbali
SAM_2770Kada maarafu kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Violet Mfuko akishow love na Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta katika usiku wa marafiki wa Lowassa iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha
SAM_2745Wacheza show wakiwa wanafanya yao stejini
SAM_2810
Mwanabloga wa libeneke la kaskazini Woinde Shiza akishow love na Deo Gee mfanyakazi wa kituo cha Radio 5 jijini Arusha

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nurdin Billal maarufu kama Shetta na mwenzake,Abdulwaheed Sykes”Dully Sykes”juzi wametangaza rasmi kumuunga mkono mgombea anayetajwa kuwania nafasi ya urais kupitia CCM mwaka huu,Edward Lowasa. Imeandikwa na Pamela Mollel wa jamiiblog.

Wasanii hao walitangaza uamuzi wao katika ukumbi wa burudani wa triple A uliopo jijini Arusha wakati walipokuwa wakiburudisha onyesho la marafiki wa Lowasa maarufu kama”Friends of Lowasa white Party”.

Akitangaza uamuzi wake,Sykes alisema kuwa yeye amemua kumuunga mkono Lowasa katika mbio za urais kwa kuwa ndiye chaguo lake tangu hapo zamani.

“Jamani mimi namuunga mkono Lowasa yeye ndiye chaguo langu tangu zamani mimi ni mfuasi wa kiongozi huyu”alisema msanii huyo na kuibua shangwe

Hatahivyo,kwa upande wake Billal alisema kuwa yeye atamuunga mkono mgombea huyo anayetajwa kuwania nafasi ya juu katika medani za siasa hapa nchini  endapo akipitishwa na chama chake.

Alisema kuwa kila binadamu ana mapenzi yake na kwa maana hiyo yeye atamuunga mkono Lowasa kwa kuwa ndiye changuo lake kwa sasa.

Katika onyesho hilo lililoanza majira ya saa 10.00 usiku watu mbalimbali kabla ya kuwasili ukumbini walipata fursa ya kupiga picha katika zulia jekundu ambapo usiku huo ulipambwa na vazi jeupe ambapo watu mbalimbali walivalia vazi hilo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top