Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FC BARCELONA WATOKA SARE NA ATHLETIC BILBAO


Baada ya miaka 31 kupita, Athletic Bilbao wametwaa kombe la kwanza baada ya kuinyuka Barcelona kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1 katika mechi mbili za fainali ya Spanish Super Cup.
Jana usiku, Barcelona wamelazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa marudiano wa kombe hilo uliopigwa dimba la Camp Nou, wakati katika mechi ya kwanza walikula kichapo cha 4-0.
Athletic Bilbao goalkeeper Gorka Iraizoz refused to let go of the ball in a bid to waste time after Barcelona opened the scoring in the first half
Lionel Messi aliwafungia Barca goli la kuongoza dakika ya 43' na kufufua matumaini ya kupindua matokeo ya awali, lakini yule yule aliyepiga ha-trick kwenye mechi iliyopita, Aritz Aduriz alifuta baadaye dakika ya 74.
Bahati mbaya zaidi, Gerard Pique alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 56, lakini dakika ya 86 Kike Sola wa Bilbao naye alionyeshwa kadi nyekundu.
Messi manages to keep his balance and the ball under control under pressure from Bilbao midfielder Benat
Hata hivyo Barca wameupiga mpira mwingi, kwani mpaka dakika 90 zinamalizika walikuwa wanaongoza kumiliki mpira kwa asilimia 73 dhidi ya 27 za Bilbao.
Msimu uliopita Barcelona walishinda makombe matatu yaani Treble.
Walitwaa taji la La Liga, Uefa Champions League na kombe la Mfalme.
Kufungwa na Bilbao kunamaanisha wamepoteza kombe la kwanza msimu huu mpya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top