Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Meninah aolewa na mtoto wa Prof. Muhongo


MENINAH CAPT
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Meninah Atick ‘Mennahladiva’ mwishoni mwa wiki aliuaga ukapera kwa kufunga ndoa na mtoto wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Abdukarim Haule.

Meninah, ambaye kipaji chake cha muziki kilianza kuonekana kupitia shindano la Bongo Star Search, ametamba na nyimbo za ‘Dream Tonight’, ‘Ka-Copy Ka-Paste’.
Mtoto huyo wa Waziri Muhongo, Peter Haule, amebadili dini na kuitwa Abdukarim Haule na harusi yao ilifanyika Kigamboni, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Licha ya wengi kumpongeza msanii huyo, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kwamba: “Usichague msichana ambaye ni mzuri duniani, chagua anayekupa furaha duniani, maisha ni mafupi na huwezi jua kesho kuna nini, fanya mazuri, asante Mungu kwa kila njia ninayopitia, nazidi kukumbuka kwa kubadilisha maisha yangu na kutumaini milele”.CHANZO:HABARI LEO 
IMECHOTWA KWENYE MTANDAO VICTOR SIMON
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top