Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA, MKOANI MBEYA


 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter  Pinda(katikati) akipokea Salaam kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza kwa Askari wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kulia) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akikagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Daraja la kwanza akiongozwa na Kamanda wa Gwaride. Sherehe hizo zimefanyika leo Agosti 15, 2015 katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akitoa cheti cha sifa kwa Mwanafunzi Mhitimu wa Mafunzo hayo, Wdr. Raymond Mgosso ambaye amefanya vizuri masomo ya Darasani(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa jukwaani akifuatilia  kwa makini Onesho Maalum la zoezi la kujihami(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
 Gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la kwanza likipita mbele ya Jukwaa kutoa heshima kwa Mgeni rasmi kwa mwendo wa haraka.
 Askari wa Kike ambao wamehitimu Mafunzo hayo wakionesha zoezi la kujihami(Self Defence).
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini hafla ya kufunga Mafunzo hayo ya Uongozi. 
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Peter Pinda akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza(wa pili kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil(wa tatu kulia) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP. Stanford Ntirundura(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top