Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya CHADEMA na UKAWA, Bw. Edward Lowassa ameendelea na kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bw.
Lowassa jana aliendelea na kampeni zake katika majimbo matatu ya Mkoa
wa Dar es Salaam ambayo ni Ukonga, Kigamboni na Mbagala
Jimbo la Ukonga
Akiwa
katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tungine, Jimbo la Ukonga,Bw. Lowassa
alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, CCM wataisoma namba kwani
Watanzania wanahitaji mabadiliko.
Alisema
anataka kutimiza ndoto yake ya kuondoa umaskini wa Watanzania kwani ana
utashi na ataweza kuuondoa kwa nguvu zote ili kuijenga Tanzania mpya
wanayoitaka wananchi.
"Nimeamua
kugombea urais ili niweze kuwatumikia Watanzania; hivyo naomba
mniamini niijenge Tanzania mpya ili kila mtu awezekuishi kwa amani na
kujituma kwenye kazi," alisema.
Aliongeza
kuwa, akiwa rais atafanya maamuzi magumu ili kuwaonesha Watanzania
maana ya mabadiliko na maendeleo yanayohitajika ambapo anayekula mlo
mmoja atakula mitatu, mwenye kanga tano awe na kumi lengo ni kuijenga
Tanzania yenye maendeleo.
Bw.
Lowassa aliahidi kuondoa ushuru kwenye zana za kilimo ili kila mkulima
aweze kunufaika na kuuza mazao yake mahali popote iwe ndani au nje ya
nchi ili aweze kujipatia kipato cha uhakika.
"Serikali
yangu itatoa elimu bure kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu,nawashangaa
viongozi wa CCM wanaposema hawawezi kutoa elimu burewakati wao
wanatembelea mashangingi ya gharama kubwa.
"Nilikwenda
Pugu kwa daladala ili kutembelea wananchi; wakaanza kuongea kwani hizi
daladala za kazi gani, mbona wao wanapandisha twiga kwenye ndege na
hawasemi?" alihoji Bw. Lowassa.
Alisema
atahakikisha matatizo ya wananchi kama alivyoyataja mgombea ubunge wa
jimbo hilo, Mwita Waitara, ambapo atayatatua ambayo ni pamoja na tatizo
la ukosefu wa umeme, umaskini, huduma mbovu za afya, ukosefu wa maji
pamoja na hali ngumu ya maisha.
Jimbo la Kigamboni
Bw.
Lowassa akiwa kwenye Jimbo la Kigamboni, alisema akiwa rais wananchi
watatumia Kivuko cha Kigamboni bure na kujenga upya mji huo ili uwe
mfano wa kuigwa.
Jimbo la Mbagala
Akiwa
Jimbo la Mbagala katika Uwanja wa Zakheem, alisema ataunda Serikali
maalumu ambayo itashughulikia matatizo ya wakazi wa jiji hilo na kuleta
maendeleo ya haraka ambayo hayajawahi kutokea.
Juma Duni Haji
Naye
mgombea mwenza, Bw. Juma Duni Haji, alisema mwaka huu,CCM lazima
waachie Serikali watake wasitake kwani miaka 50 waliyokaa madarakani
imekuwa ya dhuluma na kuwanyanyasa wananchi.
Alisema baada ya kuona wanashindwa, wameanza kuleta vurugu kwakuwaambia Watanzania kutakuwepo na vurugu baada ya uchaguzi.
James Mbatia
Mwenyekiti
wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia, alisema pamoja na CCM kumpaka matope
Bw. Lowassa, wataendelea kusonga mbele hadi waingie Ikulu, hivyo Rais
Jakaya Kikwete na Serikali yake,waanze maandalizi ya kukabidhi Ikulu.
Mbowe amvaa Bulembo, Lubuva
Akihutubia
mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kauli
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Abdallah
Bulembo kuwa UKAWA wataachiwa vitu vyote isipokuwa Ikulu ni ya
kichochezi.
Alisema
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian
Lubuva, anatetea kauli hiyo akisema ni maneno ya kisiasa na kumtaka atoe
tamko juu ya hilo kwani nchi inaweza kuwaka moto.
"Mtu
ambaye atashinda lazima apewe haki yake, Jaji Lubuva asifanye utani na
kauli za akina Bulembo, nchi inaweza kuwaka moto, wananchi wapo tayari
kwa mabadiliko hivyo wapewe haki yao," alisema.
Aliongeza
kuwa, NEC ilipaswa kukemea kauli za aina hiyo pamoja na kutoa tamko
rasmi akitumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa UKAWA, kukubaliana na
maamuzi ya viongozi wakuu wa umoja huo juu ya kusimamisha mgombea mmoja
katika kila jimbo na kata.
"Tuko
katikati ya mabadiliko hatutaki mchezo, kiongozi wa NLD, CUF, CHADEMA
au NCCR-Mageuzi katika ngazi za kata na wilaya ambaye atadharau maamuzi
yetu tutamfukuza," alisema.
Frederick Sumaye
Kwa
upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Frederick Sumaye, alisema hali
anayoiona, hakuna sababu ya CCM kubaki madarakani ambapo wanachofanya
sasa ni kuwabembeleza na kuwarubuni Watanzania ili wawape kura.
"CCM
lazima iondoke madarakani, kote tulikozunguka watu wanataka mabadiliko
wakisema Oktoba 25, mwaka huu, wachukue chao kila eneo wakidai CCM ina
kiburi," alisema.
Alisema
CCM imefilisika na kuishiwa sera ndiyo maana mgombea urais wao, Dkt.
Magufuli anajinadi yeye badala ya chama akitumia nembo za CHADEMA; hivyo
alimtaka aache kuwadanganya Watanzania.
Dkt. Makongoro Mahanga
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira ambaye alitoka CCM na kuhamia upinzani,
Dkt. Makongoro Mahanga, alisema Bw. Lowassa ndiye mwarobaini wa tatizo
la ajira.
Alisema
inashangaza kuona Dkt. Magufuli kudai ataanzisha mahakama ya mafisadi
wakati idadi kubwa ya wagombea ubunge wa CCM wamepata nafasi hizo baada
ya kutoa rushwa.
Post a Comment