Baada
ya mgogoro na mgomo uliodumu kwa zaidi ya miezi minne kati ya chuo
kikuu cha Kampala na wanafunzi wa kozi ya famasia kutokana na kutokuwa
na usajili serikali imekipa usajili wa muda ili kuondokana na mgogoro
huo.
Afisa
uhusiano wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Nsachris Mwamwaja amesema
uamuzi huo umefikiwa na bodi ya baraza la famasia ili kusaidia
wanafunzi wanaomaliza kozi hiyo waweze kutambuliwa katika soko la ajira.
Baadhi
ya wanafunzi waliokumbwa na seke seke hilo wameitaka serikali
kuhakikisha inafanya ukaguzi kwenye vyuo kujiridhisha kama kozi zote
zimesajiliwa ili kuepusha migogoro kama hiyo.
Kwa
upande wa uongozi wa chuo hicho wamesema mgogoro huo umesababisha
madhara kadhaa ikiwemo uharibifu wa mali na kutoa wito kwa serikali.
Post a Comment