Umati wa waumini wa dini ya Kiislam waliokwenda kuhiji Makka, Saudi Arabia.Wakiwa wamefunika midomo yao kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusambaa kwa njia ya hewa.
Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika swala maalumya hija.
Makka, Saudi Arabia
ZAIDI ya watu 700 waliokuwa wakishiriki
sherehe za Hijja wamefariki dunia na wengine zaidi ya 450 kujeruhiwa
kwenye mkanyagano uliotokea katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Makka
nchini Saudi Arabia.
Watu wengine wamejeruhiwa katika tukio
hilo la kukanyagana lililotokea mji wa Mina, takriban kilomita tano
kutoka mji wa Mecca. Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya
kusherehekea sikukuu ya Eid al-Adha.
Idara ya ulinzi wa raia nchini humo
imesema shughuli za uokoaji zinaendelea, ambapo idara hiyo imejitahidi
kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa mpaka sasa imeongeza askari
wa ulinzi na usalama wapatao 100,000 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.
Watu zaidi ya milioni mbili walisafiri hadi kwenye mlima Arafat jana asubuhi kwa ajili ya swala kama ishara ya Hijja.
Tukio hilo wa watu kupoteza maisha
limekuja wiki chache baada ya winchi ya ujenzi kuanguka kwenye jengo la
msikiti mkubwa zaidi duniani jijini Makka na kuua watu zaidi ya 100 na
wengine mamia kujeruhiwa.
NA DAILY MAILY
Post a Comment