Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI,Reticia Ghati Mosore akizungumza
na vyombo mbalimbali vya habari katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es
Salaam muda huu kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu katika umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutangaza kuendelea na mapambano nje ya umoja huo wa vyama pinzani.
Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, Mosena Nyambabe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatima yao ya kupambana kama wenyewe NCCR-MAGEUZI bila ya UKAWA na kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa inavibana vyama vishiriki vya UKAWA katika wagombea wa Ubunge majimboni na wagombea wa udiwani katika kata.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii .
Sintofahamu
imeibuka ndani ya chama cha NCCR-Mageuzi ambapo viongozi wake wamedai
kuwa taratibu zilizo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
zimekiukwa na kufanya chama hicho kuingia katika mgogoro wa majimbo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa
Chama hicho,Leticia Ghati Mosore amesema kuwa NCCR-Mageuzi wamezidiwa
idadi ya majimbo kutokana na taratibu nyingi kukiukwa kuanzia serikali
ya Mtaa na sasa uchaguzi Mkuu.
Mama
Mosore amesema baada ya kuona mambo hayaendi sawa, na ingawa
wataendelea kuwa UKAWA, lakini sasa wameamua kupambana wenyewe kama
NCCR-Mageuzi katika kugombea viti vya ubunge pamoja na udiwani katika
mgawanyo huo ambao amedai chama hicho kimepata majimbo pungufu ndani ya
umoja wa vyama vinavyounda Ukawa.
Amesema
kuwa ili kukamilisha ushirikishwaji kulitakiwa kuundwa kamati
zitakazoendesha uchaguzi ndani ya UKAWA na mambo mengine mengi ikiwemo
uwazi wa matumizi ya fedha, lakini hayajaweza kufanyika hivyo .
“Mchakato
wa kumpata mgombea Urais haukufuta utaratibu katika ushirikishwaji wa
vyama vyote vitakavyoweza kutambua mgombea gani anaweza kusimama katika
kupeprusha bendera ya UKAWA”, amesema Mama Mosore.
Mama
Masore pia ametaka Mwenyekiti wao Mhe. James Mbatia asiwe msemaji wa
CHADEMA wakati anakiacha chama chake (NCCR-Mageuzi) kinadhoofika, akidai
kwamba wananchi wanashindwa kututoufautisha UKAWA na CCM na wataamua
kuchagua zimwi walijualo. “Tunasisitiza upinzani wa kweli nchini hauwezi
kujengwa kwa njia za hila, kwa kukiuka taratibu za kidemokrasia,
tutachangishana ili tusafiri kwenye majimbo na kata za wagombea wetu na
kuwasaidia” alisema.
Mama
Masore amesema”Tunamshauri Mwenyekiti James Mbatia aitishe vikao vya
kikatiba haraka ili tuweze kujadiliana kuhusu hatima ya Chama
chetu.Upinzani wa kweli haujengwi kwa kuweka mbele tamaa na maslahi
binafsi kuliko taifa, na kwa kutegemea propaganda.
“Tangu UKAWA ianze, matokeo yake yamekuwa ni mabaya kwa uhai na ustawi wa Chama chetu cha NCCR”, amesema mama Masore.
Kwa
upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho,Bw. Mosena Nyambabe amesema kuwa
chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuwa ndio kinafanya
uandaji wa masuala yote bila kuwa na ushirikiano na NCCR-Mageuzi licha
kuwa na udogo katika muungano huo.
Bw.
Nyambabe amewataka wanachama wote wa NCCR-Mageuzi kushikamana katika
uchaguzi mkuu ili kupata majimbo hayo licha ya kuwepo kwa changamoto ya
kufanyiwa vurugu na Chadema. Bw. Nyambabe amehoji juu ya hatima ya
NCCR-MAGEUZI baada ya uchaguzi na UKAWA wakiwa madarakani huku
changamoto zikiwa bado hazijamalizika, akitolea mfano itakuwaje kwenye
mgawanyo wa wakuu wa mikoa ,pamoja na wakuu wa Wilaya.
Amesema
NCCR-Mageuzi imepoteza matumaini katika muungano huo ya kupata wabunge
wengi, na kusisitiza kuwa chama hicho kitakuwa na wakati mgumu bila
kutafuta ufumbuzi kukiwa bado mapema
Mgawanyo
wa majimbo ambao unaleta mkanganyiko katika UKAWA ni Chadema –Majimbo
148; CUF (Majimbo 99) ,NCCR-Mageuzi (Majimbo 12) na NLD - Majimbo
matatu.
Post a Comment