WAGOMBEA
wa nafasi za Ubunge na Udiwani katika Wilaya ya Hanang, Manyara wamedai
kutokua na imani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hanang, Felix Mabula
ambaye ni Msimamizi mkuu wa uchaguzi katika jimbo hilo.
Wagombea
hao wamedai hawana imani naye kwa kuwa Mkurugenzi huyo alikumbwa na
tuhuma nyingi za matumizi mabaya ya fedha kwenye miradi ya maji na
kuboresha miundombinu ya shule za msingi tuhuma ambazo zinazowapa hofu
haki kutotendeka chini ya msimamizi huyo.
Mgombea
Ubunge katika jimbo la Hanang kwa tiketi ya Chadema, Derick Magoma
amesema tayari wameandikia barua tume ya Uchaguzi yenye kumbukumbu namba
CDM/HAN/UT/2/239 juu ya kutokua na imani na msimamizi wa Uchaguzi wa
jimbo hilo barua waliyoiwasilisha Septemba 2 mwaka huu na kuitaka Tume
iteue msimamizi mwingine.
Magoma
amesema kuwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha zilijadiliwa katika
Baraza la Madiwani zikiongozwa na madiwani wa CHADEMA ambao ni Ndugu
Peter Lori Diwani wa Kata ya Katesh, John Farayo diwani kata ya
Endasiwold, Masala Bajuta wa kata ya Gisambalang na wengine.
“Madiwani
hao waliomtuhumu Mabula ndio wagombea na hao hao Mabula atasimamia
uchaguzi wao, tunaona kabisa kuwa haki haiwezi kutendeka na hata kama
ikitendeka hatutaamini kama imetendeka,” Amesema Magoma
Mgombea
huyo amesema kuwa Mabula anakabiliwa na tuhuma za kutumia vibaya Sh.
1.1 bilioni ambazo zimepotea na zingetumika kujenga vituo vya afya,
kuleta madawa na kusambaza huduma ya maji safi ambayo ni changamoto
kubwa kwa jimbo hilo.
Mgombea
udiwani kata ya Endasiwold, John Farayo amesema kuwa wao kama wagombea
hawana imani na Mkurugenzi huyo hivyo wameitaka tume ya uchaguzi ichukue
hatua za haraka kumteua msimamizi mwingine wa uchaguzi ili uchaguzi uwe
huru na wa haki.
Mwenyekiti
wa Chadema Hanan`g, Isack Joseph amesema kuwa chama hicho kimesimamisha
wagombea udiwani 31 kati ya kata 33 na kufafanua kuwa kutokana na
rekodi ya Mkurugenzi huyo wanahitaji msimamizi mwingine wa uchaguzi
ambaye watakua na imani naye.
Na Ferdinand Shayo, Hanang
Post a Comment