Mgombea
ubunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila
ameanguka katika matokeo yaliyotangazwa jana jioni dhidi ya mpinzani
wake wa CCM, Hasna Mwilima.
Akitangaza
matokeo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uvinza ambaye pia ndiye
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini, Ruben Mfume amesema
Kafulila alipata kura 33, 382 huku mpinzani wake wa CCM akipata kura 34,
453.
Akizungumzia
kuchelewa kutangazwa kwa matokeo katika jimbo hilo, Mfume amesema ni
kutokana na kuwepo malalamiko kadhaa toka kwa wagombea wote wawili wa
CCM na NCCR-Mageuzi ambapo mgombea wa CCM alikuwa anataka kura
zihesabiwe upya.
Mfume
amesema, mgombea wa CCM (Mwilima) alitoa madai kuwa fomu zake za
kurekodi matokeo zilionekana zimefutwafutwa kwenye kata nyingi, hali
iliyompa wasiwasi kuwa huenda matokeo yake kwenye Kata hizo yamechezewa.
Katika
madai mengine, Mfume amesema Mwilima amedai fomu zake za matokeo kwenye
kata nyingi zilionekana kusainiwa na mawakala wa chama cha mpinzani
wake (NCCR-Mageuzi), hali iliyomuondolea imani ya usahihi takwimu za
matokeo hayo.
Kwa
upande wake, Kafulila amepinga hoja ya kutaka kura zihesabiwe upya kwa
madai kuwa hakuwa na imani na waliopewa dhamana ya kuzilinda kura zao
baada ya kuhesabiwa akidai walinzi pamoja wa mkurugenzi huyo ni mawakala
wa CCM katika uchaguzi.
Kafulila
amesema kutokana na uwakala wao kwa CCM, walinzi pamoja na mkurugenzi
huyo walikuwa na uwezo wa kufanya lolote baada ya zoezi la kuhesabu kura
kukamilika na kubadili matokeo ili kuisaidia CCM kushinda.
Akizungumza
baada ya matokeo kutangazwa, Kafulila amesema hakubaliani na hatua ya
mgombea wa CCM kutangazwa mshindi kwa kuwa dosari walizolalamikia
zilikuwa hazijapatiwa ufumbuzi wala yeye hakuwa ameridhia matokeo hayo
yatangazwe.
Matokeo
ya udiwani katika jimbo hilo lenye Kata 16 yanaonyesha kuwa, CCM
kimeshinda Kata 13, vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na ACT-Wazalendo
vikijipatia ushindi katika Kata moja kila kimoja.
Post a Comment