Nyota wa filamu za Bongo, Wema Issac Sepetu akiwa na Mnamibia Luis Munana .
YAMETIMIA! Ndoa ya Miss Tanzania 2006 ambaye pia ni
nyota wa filamu za Bongo, Wema Issac Sepetu na Mnamibia Luis Munana
aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Big Brother Hotshots mwaka jana, ipo
mbioni huku kijana huyo akibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislam kwa
lengo la kuwa dini moja na Wema.
Wakifurahia jambo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio la
Mnamibia huyo kubadili dini lilifanyika hivi karibuni nyumbani kwa dada
wa Wema aitwaye Nura mwenye makazi yake, Mbezi Beach jijini Dar ambapo
dua fupi iliyohudhuriwa na baadhi ya ndugu na wawili hao ilifanyika huku
Luis ‘akitawazwa’ jina jipya la Faheem.
WALIOMSINDIKIZA FAHEEMKwa upande wa Faheem, chanzo kinasema alitua nchini juzikati akitokea nchini kwake akiwa ameongozana na kaka yake mkubwa na mjomba wake (majina yao hayakuweza kupatikana). Habari kutoka chanzo chetu cha ndani ambacho ni makini zinasema kuwa, Wema ndiye aliyemshawishi Luis kubadili dini mara baada ya kumaliza mjadala wa siku nyingi kuhusu wao kufunga ndoa au kuishi kama wapenzi tu.
WEMA ACHAGUA JINA
“Wema aliposikia Luis amekubali kubadili dini, akamchagulia jina mwenyewe. Akamwambia aitwe Faheem kwa vile analipenda tangu zamani. Tangu awali Wema alishasema akizaa mtoto wa kiume atamwita Faheem, sasa kwa sababu hajazaa naona ameamua alitumie jina hilo kwa Luis. Kwa hiyo sasa ataitwa Faheem Munana na si Luis Munana,” kilisema chanzo hicho.
KWA NINI FAHEEM AMEAMUA KUMUOA WEMA?
Chanzo: “Tangu Luis aanze kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema, amekuwa akimsifia kwamba ni mwanamke mzuri kwa sura, umbo, mwonekano kwa ujumla na kila idara hivyo kwake akaona anafaa kuwa mke wa maisha yake.
“Lakini pia alipojua Wema ni staa mkubwa hapa Bongo akajiridhisha kwamba, akimuoa anaamini atatulia kwa vile kama ni starehe anazijua zote, hakuna kitu kigeni kwake kuliko akioa mwanamke asiyejua starehe halafu akazijulia akiwa ndani ya ndoa.”
Baada ya mwandishi wetu kupata ubuyu huo, alimtafuta Wema ili kusikia kauli yake ambapo alikiri Luis kubadili dini. Pia alikiri kijana huyo kubadili jina.
WEMA ASEMA YAKE
“Ni kweli, Luis sasa ni Faheem. Nimetokea kumpenda sana kwa sababu ni kijana mzuri kuliko Diamond. Tena ni mwema, anajali na siyo mswahili kama walivyo Wabongo,” alisema Wema.
VIPI KUHUSU UZAZI?
Mwandishi wetu alikwenda mbele zaidi kwa kumuuliza Wema suala la uzazi ambalo watu wengi wamekuwa wakidai yeye ni mgumba hivyo hawezi kuzaa ambapo Wema alijibu:
“Nikishafunga ndoa na Faheem nitakuwa tayari hata kupandikiza mbegu ili nimzalie. Lakini pia naamini uzazi wangu upo ila Mungu hakupenda nizae kabla ya ndoa.”
GPL
Post a Comment