Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Dr. Magufuli amepiga Kura yake Chato


Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amepiga kura katika jimbo la Chato mapema asubuhi hii na kueleza kuwa amepata dalili nzuri alipofika kwenye kituo hicho cha kupigia kura.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Dkt. Magufuli alieleza kuna dalili nzuri za ushindi kwa upande wake hasa baada ya matone ya mvua kuanza kudondoka punde alipofika kwenye kituo hicho.

Hata hivyo, Dkt. Magufuli hakutoa maelezo kuhusu matarajio yake na maoni yake kuhusu mchakato mzima wa kampeni pamoja na kutoeleza atayapokeaje matokeo ya aina yoyote.

Alito jibu la ufupi linaloashiria kuwa  atashinda, “nitaeleza baada ya kuapishwa.”

Dkt. Magufuli aliwahimiza watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi kumchagua kiongozi wanaemtaka kwa ngazi zote za urais, ubunge na udiwani na kumtanguliza Mungu katika uamuzi wao.

“Mimi nimetimiza wajibu wagu kama raia, na nawashauri wenzangu wajihimu wakapige kura kwa kuwa hilo ndilo jukumu letu, wawachague marais, wabunge na madiwani.”


Aidha, Dkt. Magufuli alieleza kuridhishwa na mazingira ya zoezi la kupiga kura katika kituo hicho.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top