Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Nzasa wakiwa wanangoja kupiga Kura
Bado wakazi wa Nzasa wanangoja kupiga Kura
Baadhi ya wakazi wakihakiki majina yao ili kujua wanatakiwa wakae sehemu gani kabla ya kupiga kura
Ulinzi pia ukiwa umeimarishwa hali ni Shwari
Wengine wanaamua kungojea pembeni kidogo
Leo shughuli zimesimama kupisha uchaguzi mkuu
KITUO CHA KUPIGIA KURA CHA KENTON
Baadhi ya wakazi wakihakiki majina yao kabla ya kuingia kwa ajili ya kupiga Kura 2015
Baadhi ya watu wakiwa wamepanga mistari kwa ajili ya kungoja kupiga kura
Kutokana na Foleni kuchangamka Baadhi yao wanaonekana kupumzika chini
Watu mbalimbali wakingojea kupiga Kura
watu wengi kituo cha Kenton
Waliokuwa wakichati wakachati sana kuperuzi na wengine wakawa bizee bizeee na kusoma Magazeti huku wakingojea Kupiga Kura
KITUO CHA KUPIGIA KURA CHA USTAWI WA JAMII
Hapa ni Chuo cha Ustawi wa Jamii ambapo pia kuna watu wamejitokeza kwa wingi kupiga Kura
Bado wanaendelea kungojea
Wengine wamekaa wakisubili kupiga Kura
Baadhi yao wamesimama Pembeni wakingoja pia kupiga Kura
Mmoja ya wazee akiwa anasaidiwa kutembea kwenda kupiga Kura
KITUO CHA KUPIGIA KURA CHA MPAKANI A KIJITONYAMA
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupiga kura katika kituo hiki cha Mpakani Kijitonyama
Kazi zikiwa zinaendelea
Umati wa watu ni Mkubwa lakini watu wanaendelea kungoja wapige Kura
Picha zote na Fredy Njeje-Blogs za Mikoa Tanzania.
===============
===============
Kituo cha Segerea Magereza hali ni shwari Wengi wajitokeza kupiga kura
Wakazi
wa Segerea wakiwa katika foleni kwaajili ya kuendelea na zoezi la
kupiga kura katika kituo cha Magereza Segerea muda huu huku hali ya
usalama ikiwa shwari kabisa
Foleni
ikiwa bado ndefu huku mwamko ukiwa mkubwa kwa rika zote kuanzia vijana
na wakina mama na baba zoezi linaendelea vizuri mpaka sasa
Blogger
Josephat Lukaza akiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo changu
cha Magereza segerea kwaajili ya kupiga kura kumchagua kiongozi
atakayenifaa
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Wakazi
wa Segerea ambao wamjiandikisha katika kituo cha Segerea Magereza
wakiwa wamejitokeza kwa wingi muda huu katika kituo hiko kwaajili ya
kushiriki zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia
Rais, wabunge na Madiwani. Hali ni shwari hakuna vurugu wala viashiria
vyovyote vile vya vurugu japokuwa kuna changamoto za hapa na pale ambapo
mkazi mmoja ameambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kupiga kura
kutokana na namba ya Kitambulisho chake cha kupigia Kura kutofautiana
tarakimu moja tu na Namba ya kitambulisho iliyoandikwa katika karatasi
la majina ya kuhakiki. Mkazi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe
amesema kuwa anasubiri Mkuu wa kituo cha Uchaguzi Segerea Magereza
kuweza kuongea nae na Kutatua swala hilo endapo ataruhusiwa basi atapiga
kura na asiporuhusiwa basi hatopiga kura
Wakazi wa Segerea wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura
Baadhi ya wakazi wa segerea wakiwa katika foleni tayari kwa kupiga kura.Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Endelea kuwa nasi hapa tutakuletea kila kinachojiri kwenye vituo vilivyo karibu yetu.
==================
==================
PIRIKAPIRIKA ZA HAPA NA PALE KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA KUPIGIA KURA JIJINI MWANZA.
Ni
katika Vituo mbalimbali Jijini Mwanza ambapo zoezi la Upigaji Kura
limeenda vyema huku likitawaliwa na utulivu katika vituo mbalimbali vya
kupigia kura.
Na:George GB Pazzo
Katika
Mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza hakukuwa na foleni za Magari kama
ilivyozoeleka na hata shughuli nyingi zilisimama ili kupisha zoezi hili
na muda si mrefu mbivu na mbichi zitaanza kujulikana hivyo ni vyema
pande zote zikawa tayari kuyapokea matokeo kwani kwenye uchaguzi kuna
kushinda na kushinwa.
Zoezi
la upigaji kura limetawaliwa na utulivu wa hali ya juu katika vituo
mbalimbali huku hamu ya kila mmoja kushiriki zoezi hilo ikiwa ni kubwa
pia
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la kupiga kura
Kulia
ni Makoye Magige ambae ni Msimamizi Mkuuu wa Kituo cha Kitangiri Kati,
eneo la Wazi namba Moja akiw-ongea na Wanahabari juu ya zoezi la
uchaguzi katika kituo hicho ambapo amesema kuwa mambo yameenda shwari na
hakukuwa na mapungufu makubwa mbali na baadhi ya wananchi kutotambua
mapema majina yao yalipo katika Kata hiyo, japo changamoto hiyo
imeshughulikiwa mapema.
Mwenye kofia ni Aloyce Mtani ambae ni Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi cha Bismack Jijini Mwanza akizungumza na Wanahabari
Kushoto
ni Goodluck Masatu ambae niMtendaji wa Kata ya Kitangiri na msimamizi
mkuu wa Uchaguzi katika Kata hiyo akiongea na Wanahari
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na
baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na
baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na
baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Piga Kura kwa Amani
Zoezi la Kupiga kira likiendelea mapema hii leo
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na
baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Wenye mahitaji maalumu nao wamepata usaidizi kwa uzuri kabisa
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na
baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII.
Kumbuka Uchaguzi Usitutenganishe, Zingatia Amani ndiyo Watanzania wanahitaji.
credit: Kamanda wa matukio
Post a Comment