Msanii wa Bongo Flava kutoka Tanzania, Diamond Platnumz bado anaendelea kuziandika headlines kwenye kurasa za burudani nchini na Africa kwa ujumla.
Baada ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye usiku wa tuzo za MTV EMA 2015 msanii huyo wa muziki wa Bongo Fleva amekuwa akipokea pongezi mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake kwenye Instagram na pia kituo kikubwa cha burudani Africa, MTVBase Africa kilichukuwa time na kumpongeza msanii huyo kutoka Tanzania…
Kuonyesha furaha yake kwa Watanzania na kwa mashabiki wake wengi, Diamond Platnumz kapost ujumbe wa shukrani kwenye page yake ya Instagram
na pia kuwapa mashabiki wake taarifa kuwa baada ya pirikapirika za
Uchaguzi Mkuu ataanda siku maalum kwa ajili ya mashabiki wake kuweza
kupiga picha na tuzo hiyo…
>>> “Hii
sio tunzo yangu ni tunzo ya wewe na mimi maana bila kura yako
nisingeweza kabisa kushinda… naomba niwashkuru sana sana kwa kura zenu
Mashabiki zangu pendwa… wasanii wenzangu, Media, Uongozi pamoja na
familia… bahati mbaya Kutokana na harakati za uchaguzi hatuta weza kuwa
na mapokezi ila ukipita tutaandaa siku maalum kwa wote tuweze piga picha
nayo… #BestAfricanAct #BestWorldwideAct #Mtvema“<<< @diamondplatnumz.
Post a Comment