Aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Chadema kata ya Sirari na kuhamia chama cha CCM, Weng’ari Mang’era (26) amemwagiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati wakimpokea mgombea ubunge wa Tarime Vijijini(CCM), Christopher Kangoye katika uwanja wa Tarafa Sirari Wilayani Tarime.
Shuhuda
mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe ameeleza” Mbunge Kangoye
alikuwa anakwenda kwenye mkutano Uwanja wa Tarafa wakati tuko
barabarani watu wakafika na kumjeruhi kwa kumwagia
tindikali,’amesema.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Lazaro Mambosasa amesema polisi wanafuatilia kujua waliohusika na tukio hilo.
Wakati
hilo likitokea, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Tarime,
Athuman Akalama alisimamisha kampeni kwa wagombea zilizokuwa
zinaendelea Nyamongo baada ya kuibuka kwa vurugu kati ya CCM na Chadema.
Leo
asubuhi mgombea Udiwani Kata ya Matongo-Nyamongo(CCM), Daud Itembe
akiwa kwenye harakati zake za kuhitimisha kampeni zake zilizokuwa
zifanyike maeneo ya stendi Nyamongo ziliibuka vurugu kati ya wafuasi wa
CCM na Chadema.
Post a Comment