Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwafariji baadhi ya majeruhi wa ajali
mbali mbali zilizotokea katika ziara za mikutano ya Kampezi mbali mbali
za vyama vya Siasa hapa Nchini.
Balozi
Seif akiwapa pole vijana waliojeruhiwa katika ajali ya gari iliyokuwa
ikielekea kwenye Mkutano wa Kampeni wa CUF Nungwi Mkoa wa Kaskazini
Unguja Hapo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.
Mkuu
wa Kitengo cha kupokea Wagonjwa wa dharura katika Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja Dr. Juma Salum Mbwana kati kati akimueleza Balozi Seif
hatua zilizochukuliwa na Madaktari katika kuwahudumia majeruhi wa ajali
mbali mbali za mikutano ya Kampeni.
Balozi
Seif na Mkuu wa Kitengo cha kupokea Wagonjwa wa dharura katika
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Dr. Juma Salum Mbwana wakibadilishana
mawazo kwenye Wodi ya akina Mama ambao baadhi yao walipata ajali ya gari
katika Mikutano ya Kampen za Uchaguzi.
MAJERUHI
10 wanaendelea kupatiwa huduma za matibabu katika Hospitali kuu ya
Mnazi Mmoja kufuatia ajali tofauti walizopata wakati wakielekea kwenye
mikutano ya Kampeni za uchaguzi inayoendelea katika sehemu mbali mbali
hapa Nchini.
Ajali
hizo takriban zote zimehusisha zaidi vijana waliokuwa wamepanda vyombo
ambavyo vyengine vikiendeshwa kwa mwendo wa kasi na baadhi vilijaa
idadi ya abiria kupindukia mpaka.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa
kufika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwakagua majeruhi hao waliopata
athari mbali mbali zikiwemo za kuvunjika viungo na michubuko.
Post a Comment