MAREHEMU Dk Abdalala Kigoda enzi za uhai wake(Pichani)
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdalala Kigoda
aliyefariki nchini India unatarajia kuwasili leo mchana tayari kwa
ajili ya mazishi.
Ofisa
habari wa Bunge, Prosper Minja ameiambia Mwananchi kuwa mwili huo
utawasili saa nane mchana kwa ndege ya Emirates na kwenda kuhifadhiwa
kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo.
Minja
amefafanua kuwa shughuli za kuaga mwili huo zitafanyika kwenye Ukumbi
wa Karimjee kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wananchi,wabunge na
viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.
“Taratibu
zote za kuaga zitafanyika Karimjee na hapo ndipo tunategemea watu wa
kada mbalimbali watafika kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk
Kigoda”amesema Minja.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi
ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa mazishi kufanyika siku ya Alhamisi.
“Kuna
kamati maalum inayohusika na msiba nadhani ikifikia uamuzi itatoa
taarifa ila ninachofahamu mazishi yatafanyika Alhamisi nyumbani kwako
Handeni” amesema Uledi
Post a Comment