Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

NEC waacha jina la mgombea aliyejitoa Jimbo la Segerea

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CUF, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) jimbo la Segerea, Julius Mtatiro, ameilalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kulibakisha jina la Anatropia Theonest wa Chadema kwenye karatasi ya mpiga kura wa jimbo lake, wakati walishakubaliana amejitoa. 

Mtatiro alizungumza, alipokwenda kutembelea kituo cha kupigia kura cha Tabata, Kisiwani jana na kusema, kuwepo kwa jina hilo kwenye karatasi ya mpiga kura, ni makosa kwa sababu mgombea huyo alishajitoa. 

"Uchaguzi unaendelea vizuri, lakini lipo tatizo moja lililojitokeza ambalo ni kuwepo kwa jina la Anatropia Theonest kama mgombea wa Ubunge wa jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chadema wakati alishajitoa, hiyo inaweza kuwachanganya wapiga kura,"alisema Mtatiro. 

Amesema, Theonest ni wa Chadema lakini Ukawa walishakubaliana kumsimamisha Mtatiro kuwa mgombea wa jimbo hilo chini ya mwamvuli huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top