NA MWANDISHI WETU WASHINGTON
SERIKALI
ya Tanzania imetakiwa kuhakikisha kuwa amani na usalama vinakuwepo
wakati na baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini
Tanzania tarehe 25 mwezi huu.
Profesa Nicholas Boaz,
Wito
huo umetolewa na Mhadhiri wa Mawasiliano na Sera katika Chuo Kikuu cha
Maryland nchini Marekani, Profesa Nicholas Boaz katika mahojiano maalum
na Swahilivilla.
Akizungumza
na mwandishi wetu nyumbani kwake, Profesa Boaz ambaye amerejea nchini
Marekani hivi karibuni baada ya ziara yake Tanzania, alisema kuwa nchini
Tanzania kuna joto kali sana na vuguvugu la mabadiliko."Kuna joto kali
sana la uchaguzi. Kwa kweli naona watu wengi wanaitikia wito wa kutaka
mabadiliko", alisistiza profesa Boaz.
Alisema
kuwa hali duni za wananchi katika nyanja mbalimbali za maisha baada ya
miaka mingi ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na miaka kumi ya
utawala wa Rais Jakaya Kikwete, ndiyo iliyopelekea mwamko wa vuguvugu la
kutaka mabadiliko.
"Baada
ya muda mrefu wa CCM kuwa madarakani, na miaka kumi ya Rais Kikwete,
basi watu wamepata mwamko kuwa maisha na maendeleo yao yamekuwa duni.
Kwa
hivyo wanataka wapate mabadiliko ya kiongozi na kimtazamo juu ya namna
ya kuweza kuwasaidia watu hasa katika maswala ya kazi, afya, mamno ya
shule na mambo mengine mengi".
Aliyataja mambo hayo mengine kuwa ni swala la uhuru wa watu kujieleza na kuuliza juu ya kitu ambacho kinawakera.
Akijibu
swali iwapo kweli wananchi wa Tanzania wamepata mwamko wa mabadiliko au
wanaimba tu nyimbo za wanasiasa, Bwana Boaz alisema "Huwezi kuingia
akilini mwa watu kuwajua nini wanakitaka.
Lakini
ukiona watu wanakusanyika wakasema wanataka mabadiliko, kuna kitu gani
cha kuuliza zaidi ya hicho?" alidadisi msomi huyo na kuongea, "huu ni
ushahidi kuwa watu wanataka mabadiliko ya kweli"
Aidha
alisema kuwa wimbi hilo la mabadiliko linatokana na hali ya watu kukata
tamaa na ahadi zinazotolewa na viongozi wa CCM wakati wakitafuta ridhaa
ya wananchi kuingia madarakani na badala yake hali za maisha kuendelea
kuwa duni.
Aliutolea
mfano utawala wa Rais Kikwete ambaye aliingia madarakani akiwa na ari
mpya, nguvu mpya na milo mitatu kwa siku, lakini baada ya miaka kumi ya
utawala wake ukuwaji wa uchumi umebakia palepale.
"Kuna
takwimu zinaonesha waziwazi, alipoingia Kikwete 2005 kuchukua madaraka
aliukuta uchumi ukiwa ni asilimia 0.7, kwa miaka kumi, huo uchumi
umebakia palepale, na watu hawapati hata nusu mlo", alifafanua msomi
huyo na kusisitiza "Watu wameamka, hawadanganyiki tena na mambo ya
zamani ya kubebwa tu na Chama. Watu sasa hivi wanangalia jinsi ya
kuboresha maisha yao na kulinda mustakbali wa watoto wao"
Mtaalamu
huyo aliendelea kufafanua kuwa kumekuweko na takwimu za kupotosha
kuhusu ni chama gani kitashinda uchaguzi, hata hivyo alisema, "Mimi
nikiwa kama Mhadhiri na mtaalamu wa Mawasiliano na Sera, huwa
nayaangalia mambo yanavyokwenda kwa kutumia njia inayoitwa Observational
Research Method"
Alifafanua
ibara hiyo ya kitaalamu kwa kusema "Naangalia mikusanyiko ya watu
anapokuwepo Lowassa na anapokuwepo Magufuli. Kwa hiyo, unaweza kutazama
kwa hiyo tu bila hata takwimmu".
Kwa
mujibu wa utaalamu huo, Profesa Boaz anahisi kuwa upepo mwanana
unapulizia upande wa vyama vinavyojumuika chini ya mwamvuli wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Pia
alidokeza kuwa takwimu zenyewe zinabashiria ushindi kwa UKAWA. "Kuna
takwimu kutoka serikalini zinasema kuwa asilimia baina ya 60 hadi 74 ya
wapigakura wote ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 40.
Na
katika hao kuna uwezekano mkubwa vijana kuipigia kura UKAWA kuliko CCM",
alifafanua msomi huyo na kuongeza "Kwa hiyo ikiwa mambo yatakwenda
vizuri bila ubabaishaji, basi kuna uwezekano mkubwa kwa UKAWA kuchukua
nchi, lakini tarehe 25 mambo yatakuwa wazi"
Akijibu
hoja kuhusu madai ya baadhi ya wadadisi wanaodai kuwa viongozi wa CCM
waliokihama chama hicho na kujiunga na kambi ya upinzani wanatumiliwa na
chama tawala kama vibaraka wa kudhofisha upinzani, Profesa Boaz
aliimabia Swahilivilla "Watu wana uhuru wa kudadisi mambo au maoni,
lakini watu wengine wanaweza kupotosha kitu ambacho kinaonekana kina
ukweli"
Aliitupilia
mbali joja hiyo kwa kusema "Hayo ni mambo ambayo watu wanayazusha na
hayaingii hata akilini". Aliendelea kufafanua "Mimi nimetembelea sehemu
mbalimbali Tanzania, mijini na vijijini, na unakuta kitu watu
wanachokizungumzia ni mabadiliko"
Alisisitiza
kuwa Watanzania wana kiu ya mabadiliko, na kwamba kati ya watu kumi
wanaozungumza saba wanataka mabadiliko. "Unaweza kuwakuta watu kumi,
labda wawili au watatu wanazungumzia CCM, lakini saba wanazungumzia
mabadiliko na wanasema ni kwa nini wanataka mabadiliko"
Aidha
aliusifu mwamko wa wapiga kura kwa kuthamini na kuzilinda shahada zao za
kupigia kura kiasi cha kufikia kuziita "Vichinjio" na kuzionesha wakati
wanapoulizwa mikutanoni.
Aliwatolea
changamoto wale wote wanaobeza vuguvugu la mabadiliko kwa ksema
"Tusubiri tuone hiyo tarehe 25 tuone mambo yatakuwaje, je kweli hayo
mabadiliko yanayozungumzwa yatatokea? Nafikiri labda tutazame pale,
lakini joto liko na watu wanataka mabadiliko"
Akijibu
swali kuhusu malalamiko ya upinzani dhidi ya uadilifu wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), Profesa Boaz aliyapongeza mabadiliko yaliyofanywa na
Tume hiyo likiwemo swala la matokeo yote ya uchaguzi kubandikwa vituoni
tangu ya Udiwani hadi Uraisi, pamoja na vyama vyote kuruhusiwa kuwa na
mawakala wao ndani ya vituo vya kupigia kura.
"Nafikiri
hayo ni mambo ambayo yameleta faraja kuwa kuna uwazi, kwa sababu
ukileta demokrasia vitu kama hivyo vinakuwa ni vya lazima, huwezi
kufanya vitu kwa kujificha ficha"
Hata
hivyo, alielezea wasiwasi wake juu ya kauli ya Tume ya uchaguzi kwamba
wananchi wakishapiga kura hawaruhusiwi kukaa eneo la vituo vya kupigia
kura umbali wa mita 200, akisistiza kuwa hiyo ni haki ya wananchi
kikatiba. "Lakini katika katiba limo hilo, mwaka 2005 watu walikaa.
Sasa hilo ni swali la NEC kulitatua. Kwa sababu ni haki na ndiyo njia ya uwazi kuona kweli kura zetu tumepiga, tunaziona"
Alielezea
kuwa raia wa Tanzania ni watu wa amani na wasiopenda fujo, na kamwe
hawawezi kuanzisha jufo, na kwamba iwapo fujo zitatokea, basi wa
kubebeshwa lawama ni mamlaka husika.
"Kama
kuna mtu ataanzisha fujo, basi ni askari wenyewe na serikali yenyewe ya
Chama cha Mapinduzi, na mimi siamini kuwa ni watu wenyewe wataanzisha
fujo", alisema Bwana Boaz kwa sauti ya kizalendo, na kudadisi "Kwani
kuna ubaya gani, kuna kitisho gani, au CCM ina wasiwasi?"
Alifutilia
mbali madai hayo ya uwezekanio wa kutokea fujo kwa kusema kuwa viongozi
wa upinzani wamekuwa wakiwahimiza wafuasi wao kutunza amani na utulivu
kwa kusema "viongozi wao hao wa vyama vya upinzani wamewaambia,
mukimaliza kupiga kura kaeni kule pembeni, tulieni"
Aidha,
alikariri lawama zake kwa vyombo vya ulinzi na usalama na rais Kikwete
mwenyewe kwa kushindwa kuyakemea mambo hayo na kwenda kinyume na katiba.
"Fujo Tanzania ikianza, kwa kweli itakuwa imeanzishwa na askari na yeye
rais wa Jamhuri ya Tanzania ambaye alitakiwa hivyo vitu avikemee sana,
na kwamba afuate hiyo katiba, hii ndiyo maana ya sheria" alitoa dukuduku
lake na kuwa "Hili ndilo tatizo tulilonalo Tanzania, sheria zinakuwa
hazifuatwi"
Halkadhalika
Profesa Boaz alitoa nasaha kwa rais Kikwete kuwaheshimu wapiga kura
ambao ndio waliomwingiza madarakani madala ya kutumia kauli za vitisho.
"Yeye Kikwete muda wake umekwisha, mimi nadhani angekaa akatulia, aache
tena haya mambo ya kusema Polisi watafanya mambo ambayo watu hawayataki"
Alielezea
imani yake kuwa Tume ya uchaguzi itaweza kurekebisha kasoro zote kabla
ya siku ya uchaguzi. "Kwa hiyo mimi naona tusubiri mpaka Jumamosi, watu
watakuwa wamelitatua, kwa sababu watu ni haki yao kutazama", alisema
Bwana Boaz na kuhoji "Kwani kuna ulazima wakake nyumbani?
Prosesa
Boaz alimalizia kwa kutoa nasaha kwa Watanzania wote wenye haki ya
kuoiga kura kujitokeza kwa wingi kupia kura na kumchagua mtu wanayemtaka
kwa njia za amani bila woga ili kuendeleza sifa ya Tanzania kama nchi
ya amani.
"Kwa
hiyo mimi nahisi watu wakapige kura kwa amani wachague mtu wanayemtaka,
na siyo kununuliwa na mtu yoyote au kufanya jambo jengine lolote"
itafaa
kukumbusha kuwa kumekuweko na hali ya sintofahamu miongoni mwa wadau wa
kisiasa nchini Tanzania kufuatia kauli iliyotolewa na NEC pamoja na
Rais Jakaya Kikwete kwamba wananchi wakishapiga kura hawaruhusiwi kukaa
eneo la vituo vya kupigia kura umbali wa mita 200.
Hali
hiyo imepelekea imepelekea baadhi ya wanasiasa wa upinzani kufungua kesi
mahakamni anaitaka mahakama itamke kama ni halali kwa Rais na Tume ya
Uchaguzi (NEC) kuzuia wananchi kukaa kwa utulivu umbali huo ama la.
Post a Comment