SERIKALI imeeleza kushangazwa na uzushi kwamba siku ya uchaguzi mkuu, data za mawasiliano pamoja na umeme vitazimwa, jambo ambalo imetaka wananchi kupuuza taarifa hizo potofu.
Taarifa
hizo ambazo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January
Makamba ameziita ni uzushi, zinadaiwa kutolewa na baadhi ya wanasiasa
wa vyama vya upinzani wakidai kwamba serikali imepanga kufanya hivyo ili
wananchi washindwe kupata taarifa za matokeo ya uchaguzi.
“Kwanza
napenda ifahamike kuwa hakuna chama chochote cha siasa kitakachofaidika
kikiwemo Chama Cha Mapinduzi (CCM), endapo data za mawasiliano
zitazimwa, hivyo nawaomba wananchi wasiamini maneno ya uzushi yasiyo na
ukweli hata chembe,” alisisitiza January.
Alisema
huduma ya data zina umuhimu mkubwa katika uchumi wa Tanzania kuliko
siasa, kwani kwani ofisi nyingi zikiwemo taasisi za kibenki zinategemea
data hizo katika shughuli zake za kila siku.
“Sasa
ukisema tutazima data ni sawa na ku-paralyze (kusimamisha) uchumi kwani
watu hawataweza hata kutoa fedha zao benki, jambo ambalo ki ukweli
haliwezi kufanyika,” alisisitiza.
Alisema
ni Wizara yake na Serikali kwa ujumla, imekuwa ikilinda na kurekebisha
mitandao kuhakikisha inafanya kazi vizuri hasa katika kipindi hicho cha
uchaguzi kutokana na ukweli kuwa kutakuwa na taarifa nyingi
zinazohitajika kufikia wananchi.
“Hatutegemei
watu kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kusababisha taharuki lakini
hata wakifanya hivyo, Sheria ya kudhibiti mitandao ipo, itatumika
kudhibiti na si kuzima data kama inavyodaiwa,” alisema January.
Aidha
alisema taarifa hizo zilizosambazwa ambazo hata yeye ameziona,
zinasambazwa na wanasiasa wenye nia ya kutengeneza hamaki kwa wananchi
jambo ambalo si sahihi.
Wakati huo huo, msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Adrian Severine, alisema kwa sasa shirika hilo, haliwezi kuzungumzia jambo hilo, hadi pale wanasiasa wote wanaodai mtaani kuwa wanazo taarifa za kuzimwa umeme nchini siku ya uchaguzi watoe uthibitisho.
Wakati huo huo, msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Adrian Severine, alisema kwa sasa shirika hilo, haliwezi kuzungumzia jambo hilo, hadi pale wanasiasa wote wanaodai mtaani kuwa wanazo taarifa za kuzimwa umeme nchini siku ya uchaguzi watoe uthibitisho.
“Huu
ni wakati wa uchaguzi, hawa wanasiasa watasema mengi tu, sasa sisi kama
shirika hatuwezi kusema lolote wala kukanusha taarifa hizi mpaka hao
wanaodai kuwa wana taarifa kuwa tumeamriwa tuzime umeme watuthibitishie.
Siwezi kukanusha kitu ambacho hakina uthibitisho,” alisisitiza Severine.
Alisema
kwa sasa shirika hilo, limeamua watu wote watakaozusha taarifa kuhusu
utendaji au shughuli za shirika hilo na kuthibitika kuwa ni uongo,
wataburuzwa mahakamani ili iwe fundisho. “Kuna watu tayari
tumewafungulia mashitaka kwa ama kuandika au kuzungumzia taarifa za
uongo kuhusu Tanesco, kesi zinaendelea mahakamani,” alisema.
Juzi
katika mkutano wa viongozi wa siasa ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, alidai kuwa
chama hicho kinazo taarifa za uhakika kuwa siku ya uchaguzi umeme na
data vitazimwa ili wananchi washindwe kupata taarifa za uchaguzi. Pamoja
na kiongozi huyo, kutoa kauli hiyo, pia baadhi ya mitandao nayo imekuwa
ikisambaza taarifa hizo.
Post a Comment