CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimetishia kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amesema wanadhamilia
kutoshiriki katika uchaguzi huo kutokana Tume yaTaifa ya Uchaguzi (NEC)
kutokuwa na msimamo katika kazi zake.
Anasema
zikiwa zimebaki siku tatu wananchi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu lakini
NEC hadi sasa haina msimamo na kuonekana kuyapuuza madai mengi yenye
hoja yanayotolewa na Ukawa.
Akiyataja
baadhi ya madai ambayo NEC imeyapuuza ni kutotoa ushirikiano wa
kufafanua juu ya upigaji kura kwa watu ambao hawakuona majina yao kwenye
daftari la kupiga kura na kutotoa sababu ya utofauti wa namba za
kupigia kura kutoka kwenye daftari na kwenye kitambulisho.
Munisi
ameongeza kuwa, NEC wamepuuza kutoa ufafanuzi juu ya picha ambazo
haziitajiki katika upigaji kura, kutoa ufafanuzi juu ya listi mpya ya
wapiga kura iliyosemwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva,
kwamba kutakuwa na watu wa ziada ambao hawapo kwenye daftari, Je,
wanatoka wapi na wapo wangapi? Amehoji.
“Kwa
mtindo huu ambao NEC inaenda nao wa kukubali watu wasiokuwa kwenye
daftari wapige kura na hata wasiokuwepo kwenye orodha wapige kura mbona
hawakutushirikisha sisi wadau wa uchaguzi? Inaweza kupelekea uvunjifu wa
amani. Hilo ndio bao la mkono ambalo lilisemwa na hatutaki litokee,” anasema Munisi.
Munisi
amesema sababu nyingine kubwa ambayo inaweza kupelekea wasishiriki
kwenye uchaguzi ni kuhusu madudu yaliyopo ndani ya daftari la wapiga
kura, ambapo hadi sasa NEC haijatoa jibu linaloeleweka juu ya makosa
ambayo yalionekana kwenye daftari.
Sababu nyingine ya kutaka kutoshiriki amesema, “Hatuna
imani na ujumlishaji wa matokeo ya kura kwa njia ya mashine zao za
kujumlisha kwani zinamapungufu mengi. Tuliomba tume itumie njia ya
kawaida kwa njia ya kalukuleta ili kila mtu alidhike lakini walidai
tunawaingilia kazi zake. Sisi hatutakubali,” amesema Munisi.
Kwa
mujibu wa Munisi amesema, hadi sasa bado wanaendelea na uchunguzi
kwenye madaftari ya wapiga kura ambapo amesema wameshakagua katika mikoa
tisa na kubaini matatizo mengi zaidi yakiwemo ya picha hewa, picha za
watu wawili na majina ya kiume kwenye picha za kike.
“Hapo
hatujafanya katika majimbo yote tulifanya baadhi. Bado tunaendelea na
uchunguzi hadi kesho, tukiona makosa yanazidi kiwango cha kufanya
uchaguzi usiende vizuri basi tunaiomba NEC ipeleke uchaguzi mbele,” amesema Munisi.
Aidha,
ameitaka NEC kutoa orodha maalumu ya vituo vya kupigia kura kwani hadi
sasa Ukawa bado hawajajua idadi kamili ya vituo hivyo wanashindwa
kuwaapisha mawakala kwa idadi ya vituo kubadilishwa kila siku.
Post a Comment