Kaimu
Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed
Janabi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na
waandishi wa habari leo baada ya taasisi hiyo kufanikiwa kuwafanyia
upasuaji watoto 37.
Mkuu
wa Kitengo cha Moyo cha Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), Godwin Shirau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matatizo
mbalimbali ya moyo.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Profesa Mohamed Janabi leo katika hospitali hiyo.
HOSPITALI
ya Taifa Muhimbili (MNH) kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya
Shilingi mIlioni 800 baada ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto 37
wenye matatizo ya moyo .
Operesheni
hiyo imefanyika kuanzia Oktoba 10 hadi 19 mwaka huu kwa kushirikisha
timu ya wataalam 18 kutoka nchini Italy na Marekani pamoja na
madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi hiyo.
Kaimu
Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi amewaeleza waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kwamba endapo wagonjwa hao wangetibiwa
nje, kila mmoja yangegharimu kati ya Dola za Kimarekai 10,000 hadi
15,000, gharama ambazo Watanzania wengi hawawezi kuzimudu.
Kwa mujibu wa Profesa Janabi, changamoto inayowakabili ni upatikanaji wa damu na upungufu wa watalaam.
Alifafanua
kwamba hivi sasa kuna orodha ya watu 500 ambao wanasubiri kufanyiwa
upasuaji wa moyo, na kwamba desemba mwaka huu, wanatarajia kupokea
wagonjwa wenye matatizo ya moyo kutoka nchini Zambia.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto, Dk. Edwin Shiran
amesema watoto 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na wengine 20
wamewekewa kifaa maalum kwa ajili ya kuziba matundu na kuzibua mishipa
ambayo imezibana na kwamba kati ya hao watoto wawili wametokea Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Tangu Januari mwaka huu tayari wamekwishafanyiwa upasuaji wa moyo watoto 122 na watu wazima 132 .
Post a Comment