Mkuu
wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Makao Makuu ya Trafiki, Dar es Salaam,
ASP Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria, muda mfupi
kabla ya kuanza safari za mikoani katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,
jijini Dar es Salaam, elimu ambayo inalenga kudhibiti ajali za
barabarani kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Asha Adam, akiwasisitiza abiria
kufunga mikanda iliyopo kwenye viti walivyoketi muda wote wa safari
muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi ya
abiria Ubungo, jijini Dar es Salaam, kama hatua ya kudhibiti majeraha na
vifo vitokanavyo na ajali za barabarani, kuelekea kipindi cha mwisho wa
mwaka.
Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Samwi(kushoto),
na PC Elisante Bura(kulia), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari
zake mikoani, kutekeleza mkakati wa Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha
Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa
mwaka.Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka
katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa
mbalimbali ya Tanzania.
Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Swami(aliyeko
chini ya uvungu wa gari), akikagua moja ya magari yanayojiandaa kuelekea
mikoani, zoezi ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuanza
kuondoka katika kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es
Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante Bura. Hatua hii ya Jeshi
la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho
wa mwaka.
Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Sajenti Jackson Mafuru (kulia), na PC
Elisante Bura(kushoto), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake
mikoani. zoezi hili ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari
kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam, ni
moja ya hatua ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani
kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari
wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Koplo Abdallah Bwasi akikagua moja ya
magari yanayofanya safari zake nje ya mkoa wa Dar es Salaam, muda mfupi
kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini
Dar es Salaam.Hatua hii ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama
Barabarani imekuja kwa lengo la kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha
mwisho wa mwaka.(Picha zote na Abubakari Akida, Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi).
Post a Comment