Mkuu
wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti
vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani. Mkuu
wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Giveness Aswile, akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo, kuvishukuru vyombo vya habari kwa kuripoti
vizuri katika kipindi chote cha uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani.
Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Emmanuel Kavishe.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imesema kuwa waandishi wamechangia kufanya
uchaguzi kuwa haki na uhuru kutokana na kutoa taarifa zao bila kuegemea
upande.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya
sheria wa NEC, Emmanuel Kawishe amesema kuwa mwenendo wa uchaguzi tume
ilifanya kuwa wazi kwa kuhakikisha wananchi wanapata habari kupitia
vyombo habari.
Amesema
kuwa NEC haina uwezo wa kufikia watu milioni 26 kutokana na kuwepo kwa
vyombo vya habari kwani vimekuwa ni daraja la kufanya wananchi wafikiwe
na habari kwa wakati.
Kawishe
aliongeza kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi amekuwa akishiri
katika vyombo habari katika kutoa taarifa kwani bila kufanya hivyo zoezi
la upigaji kura lisingekuwa rahisi kama wananchi wasingepata elimu ya
mpiga kura.
’’Upigaji
wa kura umeisha napita kwa kujidai na watu wengi wananikaribisha katika
kushiriki hata kunywa kahawa nisingefanya hivyo kama vyombo vya habari
vingeongea vibaya kuhusu mimi juu ya elimu niliyokuwa nikitoa katika
vyombo hivyo.’’amesema Kawishe.
Nae
Mkuu wa Idara ya Habari NEC, Giveness Aswile amesema katika uchaguzi
ujao watajipanga waandishi waweze kufika sehemu zote ili wananchi wajue
kazi za tume.
Amesema
Tume imekuwa wazi na kufanya waandishi wajitume katika kutoa taarifa
ambazo zimefanya uchaguzi kuwa wa wazi na huru zaidi kwa kupata habari
katika kila hatua ambayo tume ilikuwa ikifanya.
Post a Comment