Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale- Mwiru amesema atazungumzia mchakato wa Uchaguzi Mkuu baadaye baada ya kukusanya taarifa za kutosha.
Akizungumza
kwa njia ya simu baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu Uchaguzi Mkuu
uliomalizika hivi karibuni na Dk John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kutangazwa mshindi, Kingunge bila kufafanua zaidi alisema: “Nitazungumzia mchakato wa uchaguzi baadaye baada ya kukamilisha kukusanya taarifa.”
Mwanzoni
mwa Oktoba, Kingunge ambaye amekuwa kada wa CCM kwa miaka 61 (tangu
enzi za TANU), alitangaza kujitoa katika chama hicho akisema hawezi
kuendelea kuwa ndani ya chama kinachoendeshwa kwa maslahi binafsi.
Kingunge
ambaye amefanya kazi kwa karibu ndani ya CCM na Serikali na marais wa
wote wa awamu nne, alidai chama hicho kimepoteza mwelekeo na hakijadili
mambo muhimu kama ilivyokuwa zamani.
Pamoja
na Kingunge kudai hajiungi na chama kingine chochote cha siasa,
alionekana kwenye jukwaa la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wakati wa kumnadi mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho aliyeungwa na
vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.
Uchaguzi
Mkuu ulifanyika Oktoba 25, mwaka huu, na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
ilimtangaza Dk John Magufuli kuwa mshindi baada ya kupata kura 8,882,935
(asilimia 58.46) na kufuatiwa na Lowassa kura 6,072,848 (asilimia
39.97).
Post a Comment