Daraja
lililokuwa linawasumbua mno wakazi na wananchi wa Mbweni JKT, sasa
linaelekea mwishoni, hali iliyoanza kuwafurahisha wananchi hao waliokuwa
wakisumbuka kuvuka eneo hilo lililokuwa linajaa maji mara kwa mara
yanayotoka baharini.
Katika pita pita ya mitandaoni, tuliona picha hizi ambazo tayari zimeshapokewa kwa shangwe kutokana na wananchi hao kuanza kulitumia. Ikumbukwe kwamba kutokuwapo kwa daraja hili kulileta usumbufu mkubwa kwa wananchi.
Kabla
ya uwapo wa daraja hili, magari yalilazimika kupita kwenye maji na
pengine yanapokuwa mengi kushindwa kuvuka. Ni kutokana na daraja hili,
shukrani za dhati ziende kwa JKT wanaojenga daraja hili, serikali Kuu
kwa kupitia Mkuu wa Wilaya Kinondoni, DC Paulo Makonda na watendaji wote
waliohakikisha kwamba utengenezaji wa daraja hili unakamilika ili
kuondoa adha kwa wakazi na wananchi wa Mbweni JKT.
Mkazi mmoja wa Mbweni aliyeshindwa kutaja jina lake alitumia muda mwingi kuwasifu wahusika kwa kulisimamia vyema daraja hilo litakalokuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo na wote wanaoishi jijini Dar es Salaam.
Picha ya daraja hili la Mbweni JKT ilipigwa kwenye gari.
Post a Comment