Na Rabbi Hume
Serikali
nchini, kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ipo mbioni kufanya
mazungumzo na wamiliki wa maduka ya madawa yaliyopo pembezoni na
hospitali za serikali ili kuona uwezekano wa kuhamisha maduka hayo
kutoka maeneo ya hospitali ilikuondoa utata uliopo sasa wa baadhi ya
watendaji na wafanyakazi wa hospitali hizo kutumia mwaya huo wa
kuhamisha madawa na kuweka kwenye maduka hayo.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt.
Donald Mbando wakati akizungumza na waandishi mapema leo jijini Dar es
Salaam, kuhusu ziara aliyofanya katika baadhi ya hospitali zilizopo hapa
nchini ikiwemo jiji la Dar Es Salaam na kuweka wazi mipango hiyo ya
Serikali ya kuhamisha maduka hayo.
Mbando
amesema kuwa kuamishwa kwa maduka hayo kutasaidia kupunguza ukosefu wa
madawa katika hospitali za serikali ambapo kumekuwa kukihisiwa kuwa kuna
baadhi ya wafanyakazi wa hospitali wamekuwa wakizuia upatikanaji wa
dawa hospitalini ili wagonjwa waende kununua dawa hizo katika maduka yao
yaliyo nje ya hospitali.
“Tayari
tumepanga mkakati ili tuweze kuzungumza na wamiliki wa maduka ya madawa
ili waweze kuhamisha maduka hayo kutoka maeneo ya hospitali za serikali
na hilo agizo lazima litimizwe maana hata usajiri wa maduka yao upo
kiserikali,” amesema Mbando.
Aidha
pamoja na mkakati huo wa kuamisha maduka hayo pia Katibu mkuu huyo
ameyagiza hospitali zote nchini kufungua maduka ndani ya hospitali
ambayo yatawawezesha wagonjwa kununua dawa hapo hapo hospitali na
kuipongeza hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa kufungua maduka matatu na
moja likitoa huduma masaa 24.
Post a Comment