Na Nathaniel Limu, Singida
MWANAJESHI
mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) mkazi wa kijiji cha Ighuka
wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Selemani Juma Karani (64),amehukumiwa
na mahakama kuu kanda ya Dodoma adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
Karani
amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumpiga
mshale wa sumu jirani yake Hadija Swalehe kichwani upande wa kulia, na
kutokezea sikio la kushoto na kusababisha kifo chake.
Mwendesha
mashitaka wakili wa serikali mwandamizi,Seif Ahmed,amedai mbele ya
msajili mkuu wa mahakama kuu kanda ya Dar-es-salaam mwenye mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji Huruma Shaidi,kuwa mnamo februari 10 mwaka
2009 saa tisa alasiri,mshitakiwa Karani kwa makusudi,alimpiga jirani
yake mshale moja kichwani.
Mwendesha mashitaka huyo alisema kuwa mshitakiwa ametenda kosa hilo huku akijua wazi kuwa , kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Seif
alisema siku ya tukio,mshitakiwa Karani akiwa amebeba upinde na mshale
moja,alienda nyumbani kwa jirani yake Hadija, na alipomkuta bila
kusalimia au kuzozana,alinyanyua upinde wake na kumpiga kichwani.
Alisema
kuwa Hadija aliweza kukimbilia kwa jirani yake Rehema Abdala na
kumwomba amtolee mshale huo,lakini Rehema alimshauri amkimbize kituo cha
afya Ikungi kwa madai yeye asingeweza kuutoa.
“Wakiwa
njiani wanamkimbiza Hadija kituo cha afya Ikungi,alifariki dunia.Hata
hivyo walimfikisha katika kituo hicho cha afya kwa lengo la kutolewa kwa
mshale huo”,alisema mwanasheria huyo mwandamizi wa serikali.
Seif
aliiambi mahakama hiyo kwamba mashahidi wote wamedai kuwa hawakuwahi
kusikia ugomvi wo wote kati ya mshitakiwa na Hadija, na kwamba mauaji
hayo yanahusishwa na masuala ya ardhi na ushirikina.
Mmoja
wa mshahidi katika kesi hiyo, Fatuma Alli, aliiambia mahakama hiyo kuwa
siku ya tukio alikuwa nyumbani kwa Hadija wamejipumzisha.
Akifafanua,alisema
ghafla Karani aliingia na alipowakuta,hakuzungumza cho chote alinyanyua
upinde wake nakumlega Hadija na kasha kumpiga mshale moja na kisha
kuondoka kimya kimya.
Mshitakiwa
Karani akijitetea kupitia kwa wakili wake wa kujitegemea kutoka Dodoma
mjini,Mwigulu Simon,alikana kutenda kitendo hicho na kudai kwamba siku
ya tukio,alikuwa Makiungu hospitalini akipatiwa matibabu.
Akitoa
hukumu hiyo,msajili huyo,alisema ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka,umethibitisha bila kuacha shaka yo yote kwamba mshitakiwa ana
hatia kama alivyoshitakiwa.
“Kosa
la kuua kwa kukusudia,adhabu yake ni moja nayo ni kunyongwa hadi kufa
kwa mujibu wa sheria ya 196 kanuni ya adhabu sura 16.Hivyo mshitakiwa
Karani mahakama hii kuu,inakuhukumu adhabu ya kuonyongwa hadi
kufa”,alisema msajili huyo mkuu.
Post a Comment