Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemshambulia kwa maneno makali mwanasiasa mkongwe wa Kenya ambaye pia ni kiongozi wa chama cha CORDS huku akimpiga marufuku kukanyaga ardhi ya nchi hiyo.
Akizungumza
huko Marondela katika hafla iliyowahusisha wanajeshi walioshiriki
katika vita mbalimbali, Mugabe alimtuhumu Raila kwa kutaka kumpindua
kwenye nafasi yake kwa kuwapandikiza wapinzani nchini humo.
Hivi ndivyo alivyosema:
“Raila Odinga ni
mwanasiasa muongo wa Kenya, mwanaume mnafiki ambaye yuko katika mkakati
wa kuwapandikiza marafiki zake kuwa marais kwenye nchi zote za Afrika
ili awe mwenyekiti mwenye nguvu kwenye Umoja wa Afrika (AU), siku moja
watamuangusha kwenye sanduku la kura.
“Angalia alichokifanya Nigeria, Tanzania,
Ivory Coast na anataka kufanya hivyo pia Uganda kwa kumtumia rafiki
yake Kiiza Besigye ambaye leo anapewa sifa na ushupavu ambao anapata
kutokana tu na amri za Raila barani Afrika.
“Hapa
hatutamruhusu kuwageuza marafiki zake wa zamani Tendai Biti na Morgan
kuniondoa mimi, hakuna kwa namna yoyote. Nitatawala kwa miaka 90 zaidi.
Nimekiamuru kikosi maalum cha jeshi kuangusha ndege yoyote itakayokuwa
imembeba huyo mwendawazimu Raila na kundi lake la mipango ya uchakachuaji wa kura dhidi ya marais wanaoendelea kutawala Afrika.
“Nimewaamuru walinzi wangu kuhakikisha wanakuwa makini kuhakikisha Raila hajipenyezi bila kubainika.
“Tutashindwaje kukosa usingizi kwa sababu tu ya Raila, yeye ni kitu gani? Tutamkamata na kumhasi kabla yeye na timu yake hawajamsaidia Morgan na Biti kunipindua kwenye Urais.”
Hii
sio mara ya kwanza kwa Mugabe kushambulia Kenya kwa maneno, wiki chache
zilizopita alidai kuwa wananchi wa Kenya ni wezi kutoka damuni na
kwamba anadhani wanasomea shahada ya wizi. Alitahadharisha wananchi wake
kutokubali kukaa karibu na wakenya kwa madai kuwa wanaweza kuwaambukiza
wizi.
Mwezi
Juni mwaka 2008, Raila Odinga aliwasilisha pendekezo lake mbele ya
Umoja wa Afrika akitaka Umoja huo kumsimamisha uanachama Rais Mugabe
hadi pale atakaporuhusu uchaguzi huru na wa haki nchini kwake.
Post a Comment