KWA
sasa huwezi kutaja maendeleo ya muziki wa kuchana kwa kina dada bila
kumtaja mwanadada Nicki Minaj. Nicki ambaye unaweza kusema ndiye ‘top’
wa muziki wa hip hop kwa sasa ulimwengu amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
sana kuwafanya wadada nao waingie kwenye muziki huo.
Tangu
alipoachia ngoma yake ya kwanza iliyomtoa ya Your Love, hakika Nicki
aliweza kuwateka mamilioni ya wadada ambao nao walijikuta wakivutika kwa
kiasi kikubwa kurap.
Kibongobongo
pia zamani kuanzia mwishoni mwa miaka ya 90 waliibuka wadada kadhaa
ambao nao walikuwa wanachana, lakini kwa kuwa muziki wa aina hiyo
ulionekana kuimbwa zaidi na wanaume baadhi walionekana kukata tamaa
mapema.
Lakini
hata hivyo wengine walikatishwa tamaa zaidi baada ya kuona kazi zao
hazilipi kama vile ambavyo walikuwa wakitoa fedha kwa ajili ya
kutengeneza kazi zao.
Pengine
sasa hivi ambao bado wanakomaa na ‘game’ ya hip hop kwa kina dada ni
Witness, Chiku Keto na dogo ambaye anakuja kiasi chake anafahamika kama
Chemical.
Wafuatao
ni baadhi ya kina dada ambao walikuwa wanachana hatari lakini leo hii
hawasikikiki kabisa kwenye spika za redio na runinga kwa kifupi ni kama
imebaki stori;
Zay B
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 ukizungumzia muziki wa hip hop kwa upande wa
kina dada hakika ulikuwa huwezi kuliacha jina la mwanadada huyo ambaye
kiuhalisia anaitwa Zainab Lipangile.
Zay
B aliwika zaidi na Ngoma ya Gado remix aliyofanya na Juma Nature lakini
sasa amebaki stori tu kwani hajatoa wimbo wowote uliofanya vizuri kwa
muda mrefu sana na inawezekana asirudi tena na kuwika kama zamani.
Ukiachana na ngoma hiyo, bifu kati yake na Sister P lilizidi
kumng’arisha dada huyo na mwenzake kiasi cha kuandaliwa shoo ili
kumtafuta mkali zaidi.
Sister P
Anakuja anakuja Sister P! Anakuja anakuja ngangari! Enzi hizo wakati
michano ya ada huyu ambaye jina alilopewa na wazazi wake ni Happy Pella
ipo kitaani ikichana spika za raia wanaopenda burudani hakika
alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukusanya nyomi kwenye shoo zake na hicho
kilikuwa kipindi chake cha mavuno.
Sister
P aliwika na Ngoma ya Anakuja ambapo alisimama peke yake mwanzo mwisho
hivyo alionyesha uwezo mkubwa lakini leo hata ukiomba wimbo wake wowote
kwenye redio lazima ‘presenter au hata DJ itabidi aweke kwanza
‘headphone’ chini kisha aanze ‘kusambalua’ makablasha ili aweze kumpata.
Leo
hii ni ngumu kusikia ngoma zake kali kama Hey Dj, Achana Nao aliofanya
na Ally Choky na nyinginezo kibao! Wadau wamekumis rudi Sister P.
Dataz.
Dataz
Mrembo huyu alizaliwa mwaka 1984 huko Mbamba Bay, Nyasa, anaitwa Dataz
ambaye jina lake halisi ni Florence Kasela. Wimbo uliomtambulisha
uliitwa Mume wa Mtu ambapo alifanya na mwanadada ambaye pia ni muigizaji
anaitwa Joan. Ngoma hiyo ilitikisa vibaya na kumtambulisha kama kipaji
kingine chenye uwezo wa kuchana.
Sasa
hivi Dataz hasikiki tena licha ya kuwa kuna kipindi alikuwa akifanya
kazi kwa kushirikiana na kaka yake, Squeezer. Mwaka 2010 kidogo
alionekana kama angerudi baada ya kushirikishwa na Steve RnB katika
ngoma iliyoitwa Sogea Karibu ambapo alichana vizuri na wimbo ulifanya
vizuri.
Baada
ya kusikika kwenye kolabo hiyo hakuonekana tena kitaani wala kwenye
runinga na redio labda kwa media zenye vipindi vya ‘zilizobamba’ ndo
anaweza kusikika kwani alikuwa mkalii.
Rah P.
Rah P
Fredinah Peyton maarufu kama Rah P, ni dada alikuja ghafla na kutoka na
Ngoma ya Hayakuhusu ambayo kwa kweli ilifanya vizuri sana, katika listi
ya ngoma kali hii nayo ipo.
Baada
ya kutoka kimuziki dada huyo alijichanganya lakini ghafla akapotea moja
kwa moja mpaka leo huku akiacha msemo wa ‘hayakuhusu’.
Post a Comment