Aliyekuwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda
akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa ofisi ndogo za
Bunge jijini Dar es Salaam kuhusiana na kuachana na uongozi katika
siasa.
ALIYEKUWA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda
amejing'atua rasmi na kuachana na uongozi katika siasa kutokana na
kufanya kazi za Siasa kwa miaka 40.
ameyasema hayo alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam leo.
Anne
amesema kuwa "Sitagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wala sitachukua fomu ya kugombea nafasi ya uspika
wala sifikilii kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika"
Aidha
Anne amesema kuwa katika awamu yake ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo na
wabunge vijana.
Hata
hivyo kuwa na changamoto nyingi ila amesema kuwa alilifurahiya sana
Bunge hilo kutokana na kuwaelewa wabunge mbalimbali tabia zao hasa
wakiwa Bungeni.
Anne
amepsema kuwa Spika wa sasa atakaye shinda nafasi awe si mwepesi wa
kukasirika kutokana na changamoto atakazo zipata Bungeni wakati
wakijadilia masuala mbalimbali ya Serikali, pia awe mtulivu na
kukabiliana na changamoto zitakazo jitokeza.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Anne Makinda leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Post a Comment