SERIKALI
imewaagiza watendaji wa Halmashauri zote za jijini Dar es Salaam
kusimamia ipasavyo suala la usafi katika maeneo mbalimbali ili kusadia
kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu.
Katika
agizo hilo la Serikali ametoa wiki mbili kwa watendaji wote
kuhakikisha wanaliweka jiji katika hali ya usafi na endapo
halitatekelezwa hatua zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza
na watendaji wa Serikali leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu, Ofisi
ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne
Sagini, amesema kuwa utekelezaji wa malengo waliyokuwa wamejiwekea tangu
2013.
“Mlipuko
wa ugonjwa wa kipindipindu umekuwa janga, kutokana na uchafu kukithiri
katika jiji na kusababisha watu kupoteza maisha na wengine kuendelea
kuugua,”alisema Sagini.
Pia
amewataka watendaji wa halmashauri kuwatengea maeneo maalum ya kufanyia
biashara, mama lishe na baba lishe badala ya kuwafukuza.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es
Salaam(Dawasco), Mhandisi, Cyprian Luhemeja, alisema kipindupindu
hakiwezi kumalizika jijini hapa kama Halmashauri hazitashirikiana na
Dawassa na Dawasco.
Alisema
kutoshirikiana kwa halmashauri na mamlaka za maji, kuna sababisha
ujenzi holela ambao unapita katika miundombinu ya maji taka.
Pia
alisema changamoto kubwa ambayo watu wengi hawaitambui ni kuhusu
wasambazaji wa maji majumbani ambao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha
kipindupindu.
“Wasambazaji
hawa wamekuwa wakati mwingine wanasafisha maji taka na kuyasambaza
majumbani jambo ambalo linasababisha magonjwa hayo.
Kutokana na hali hiyo sisi kama DAWASCO hatutamruhusu mtu kusambaza maji kama hana kibali maalumu kilichotoka kwetu,”alisema
Post a Comment