Na Chalila
Kibuda,Globu ya Jamii.
JESHI la
Polisi limewetaka wananchi kuendelea na utulivu kama walivyoonyesha wakati wa
upigaji kura na hatimaye kupatikana katika siku ya uapishaji wa Rais Mteule
Dk.John Pombe Magufuli.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi
hilo,Paul Chagonja amesema kuwa jeshi la polisi limeridhishwa na utulivu
uliokuwepo wakati wa upigaji kura.
Amesema kuwa
utulivu huo umeweza kufanya uchaguzi kwenda salama na hatimaye kupelekea kupatikana kwa mshindi.Amesema
katika suala la Zanzibar liko katika mazungumzo hivyo viongozi wanafanya kazi
yao, hivyo maandamano hayana nafasi kutokana na taratibu wanazozitumia.
Chagonja
amesema watu waliokamatwa katika vurugu za uchaguzi wamefikishwa mahakamani na
huku wengine wakiendelea na uchunguzi,
Amesema hali
ya amani ipo na wananchi wametakiwa kulinda hali hiyo na ikitokea mtu analeta
uchochezi walipoti ka vyombo vya usalama ili hatua zichukuliwe.
Chagonja
ametaka baadhi ya taarifa katika mitandao ya jamii kuupuza taarifa ambazo
zinatoa taharuki kwa wananchi kutokana na hizo taarifa wanazotoa zinapotosha.
Post a Comment