Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akionyesha huduma mpya ya "Airtel TV" inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo
itakayowawezesha wateja wa Airtel kuangalia vipindi katika vituo
mbalimbali vya television kupitia simu zao za mkononi, akishuhudia ni
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati wa
uzinduzi wa huduma mpya ya "Airtel TV" itakayowawezesha wateja wa
Airtel kuangalia vipindi katika vituo mbalimbali vya television
kupitia simu zao za mkononi.
* Kuunganishwa na chanel 8 za ndani na nje
* Kujiunga na vifurushi vya kuangalia TV bila kikomo vya siku, wiki na mwezi
Dar es Salaam, Tanzania 19 Novemba 2015, kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imezindua huduma ya ziada itakayowawezesha wateja wake nchi
nzima kuangalia vipindi vya televisheni katika vituo vya ndani na nje
ya nchi kupitia simu zao za mkononi.
Huduma hii mpya ijulikanayo kama "Airtel TV" imeunganishwa na vituo 8
za televisheni vya ndani na nje ya nchi na kuwawezesha wateja wa
Airtel kuangalia vipindi vilivyopita katika tamsilia wanazozipenda,
kuangalia sinema na video wanazohitaji kupitia simu zao.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa "Airtel TV" Meneja Uhusiano wa Airtel ,
Bw Jackson Mmbando alisema "kwa kawaida mara nyingi watanzania
wanaangalia vipindi vya televisheni wakiwa nyumbani wakati wa jioni
baada ya kutoka katika kazi zao. Tunazindua huduma yenye gharama nafuu
itakayowawezesha wateja wetu kupata taarifa pindi wasipokuwapo
majumbani mwao.
"Airtel TV" itawapatia uzoefu wa kipekee na
kuwahabarisha wateja wetu wakati wowote wakiwa katika shughuli zao au
kwenye foleni, bila kikomo kupitia simu zao za mkononi"
" huduma hiii imelenga kukidhi mahitaji ya wateja kwa kuwapatia habari
kiurahisi kwa kujiunga na kifurushi cha siku , wiki au mwezi.
Tunaamini huduma hii itapunguza uwiano wa watu wasiokuwa na fursa ya
kuangalia Televishoni na pia kuwawezesha kupata matukio kwa wakati
kupitia simu zao mahali popote pale walipo" aliongeza Mmbando
Akiongea kuhusu mahudhui na jinsi ya kujiunga na huduma hiyo, Meneja
huduma za ziada ,Prisca Tembo alieleza zaidi kuhusu dhamira yao ya
kutoa huduma yenye kiwango cha juu na gharama nafuu.
" tunayo furaha kuwawezesha watanzania kuangalia vipindi vya televisheni kupitia simu
zao kwani tunaenda sambamba na mpango wa serikali wa kidigitali wenye
lengo la kuwa na jamii kupata taarifa za yanayotokea ndani na nje ya
nchi kwa wakati na kiwango cha juu.
Tembo aliongeza kwa kusema ili kupata huduma ya "Airtel TV" mteja
anatakiwa kupakua au kudownload application kwa kupitia linki ya
https://goo.gl/iSvaJC kwa simu za Android na https://goo.gl/IMvzCt
kwa simu za IOS.
Baada ya kuzi download mteja ataweza kununua kifurushi cha internet
maalum cha Televisheni kwa kupiga *148*88# tozo za kujiunga ni Tshs
499 kwa siku, Tshs 2,999 kwa wiki naTshs 11,999 kwa mwezi. Vituo
vinavyopatikana katika "Airtel TV" ni pamoja na Star TV, TBC, Fight
Box, 360 tune box, Citizen, FilmBox, Channel Ten na Aljazeera.
Post a Comment