Msanii wa Bongo fleva, Rich Mavoko (kushoto) akisaini Mkataba wa kujiunga na lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyopo chini ya staa wa tasnia hiyo, Diamond Platnumz (kulia).
Habari ikufikie popote ulipo wewe mpenda burudani na mdau wa muziki wa bongo fleva kuwa, leo June 2, 2016 lebo ya muziki ya Wasafi Classic Baby (WCB)inayomilikiwa na staa wa tasnia hiyo Diamond Platnumz inaingia kwenye headlines za Bongo Fleva baada ya kumtambulisha rasmi msanii wao mpya Rich Mavoko ambaye anakuwa ni msanii wa nne atakayesimamiwa kazi zake katika lebo ya WCB.
Kwa mujibu wa CEO wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz amesema…’Kwasasa Label yangu inakuwa na jumla ya wasanii nne ukiachana na Rich Mavoko kuna Dada yangu Queen Darling ambaye sijawahi kumtambulisha lakini anakuwa ni msichana wa kwanza katika label yangu kwahiyo tutakuwa na jumla ya wasanii nne Raymond, Harmonize, Rich Mavoko na Queen Darling’– Diamond Platnumz.
Post a Comment