Loading...
SAKATA DAWA ZA KULEVYA ... Askofu Gwajima afunguka mazito kanisani
Askofu Gwajima: Askari walipekuwa nyumba yangu chumba hadi chumba lakini hawakukuta kitu chochote.
Askofu Gwajima: Polisi wale hawawezi kuzungumza sababu wataonekana ni waasi. Mimi namuomba Rais aingilie kati hili suala watu wanateseka.
Gwajima: Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.
Askofu Gwajima: Mimi nitawaambia kitu, msilaumu Polisi wala Ofisi ya Rais. Wao hawahusiki na hili ila ni kiumbe mmoja tu ameibuka katikati.
Askofu Gwajima: Sijawahi kuvuta sigari, kunywa pombe wala kwenda disko tangu nimezaliwa mimi.
Askofu Gwajima: Polisi nao wanateswa kama tunavyoteswa sisi. Wanaambiwa wakapekuwe nyumba yangu japo wanajua hamna kitu ila inabidi waende.
Askofu Gwajima: Kamanda Sirro akaniuliza kwa nini nimewekwa kwenye orodha hiyo, nikamwambia ni chuki tu za mtu aliyekaa kwenye kiti chake.
Askofu Gwajima: Waliniambia wakanipime kwa Mkemia na walinipima kwa uwazi kabisa. Niliwaambia hata wakikuta pombe wasema ni dawa za kulevya.
Askofu Gwajima: Baada ya kukosa walichokuwa wanatafuta nyumbani kwangu tukarudi polisi usiku ule ule kuendelee na mahojiano.
Askofu Gwajima: Chumba nilichowekwa polisi nilikuwa mimi na manji. Nikasema 'kumbe na mimi nina pesa kiasi hiki hadi nawekwa na huyu?'
Askofu Gwajima: Sheikh Mkuu na yeye badala ya kutetea taratibu zifuatwe anamuunga mkono swaiba wake, wanampango gani hawa?
Askofu Gwajima: Manji ana kampuni 23, na ameajiri watu zaidi ya 5000. Unashindwaje kumpelekea hati ya kumuita umhoji kabla ya kumtangaza?
Askofu Gwajima: Mimi ninajua chakumfanya Makonda, mapepo yaliomba kuingia kwa nguruwe, ila sasa nitayaambia pakwenda maana nguruwe ni nyama.
Askofu Gwajima: Mapolisi 12 wamewekwa kule ndani wamejikunyata hawana mtetezi, eti Makonda ameunda tu, yani kesi ya ngedere iko kwa nyani!!
Gwajima: Lengo la Paul Makonda ni kuchafua majina ya watu kwa sababu anazozijua mwenyewe.
Askofu Gwajima: Unawaita watu waje wakuone, hata kama walikuwa na madawa si wataficha. Ndio maana nasema juhudi hizi si za dawa za kulevya.
Askofu Gwajima: Kwanini kina Manji wao hadi leo hawajafanyiwa kama nilivyofanyiwa mimi ili nao watoke mule ndani?
Askofu Gwajima: Namuomba Rais Magufuli asiache kuamini vijana kwa sababu ya huyu mmoja, kichaa aliyeharibu. Wapo vijana wenye akili nzuri.
Askofu Gwajima: Rais Magufuli vita ya dawa za kulevya isikome lakini njia hii iliyotumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam si sahihi, ni ya ovyo na ya kijinga
Askofu Gwajima: Vitu vingine huhitaji kufundishwa darasani, ni akili za kawaida tu unatakiwa kuwa nazo.
Askofu Gwajima: Namuomba Rais awaangalie wale walioshikiliwa kule mahabusu, nimewaacha hawana mtetezi, kama wanakosa hatua zichukuliwe.
Askofu Gwajima: Kesho nitarudi tena kuwaona wale watu niliowaacha. Ninaamini sasa rais anahitaji msaada wangu.
Askofu Gwajima: Mimi sikubali kama Makonda ataendelea kuwa Mkuu wa Mkoa.. Hana uwezo na hafai kabisa kwa nafasi hii.
Askofu Gwajima: Hii vita imemshinda Makonda labda akipelekwa CCP anaweza akafaa kuwa Polisi.
Askofu Gwajima: Makonda ni kombora ambalo halijaelekezwa pakutua, linaweza kutua sehemu yoyote.
Askofu Gwajima: Kuanzia sasa mtu yeyote akiona jambo halipo sawa aniambie nitapaza sauti itapita mageti yote hadi kumfikia rais na atatenda... Hatuwezi kuongozwa na vichaa kama huyu Makonda.
Askofu Gwajima: Rais Magufuli ana hekima, anaweza akaona kitu hakipo sahihi lakini akakaa kimya akuone mwisho wako, au nani amekutuma.
Askofu Gwajima: Mimi umenitangaza, ukakuta sina dawa za kulevya, kesho ukiniita kwako usifikirie nitakuja, nitakuaminije?
Askofu Gwajima: Mimi ni kama mbegu, ukinifukia ukienda ukirudi unakuta ni mti umechanua vizuri na una matunda.
Askofu Gwajima: Mamlaka aliyopewa Makonda si sahihi, nawaomba msikubali Makonda aendelee kuwa Mkuu wa Mkoa, lakini msifanye fujo.
Askofu Gwajima: Rais Magufuli tunakuunga mkono kabisa kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya, lakini njia aliyoitumia Makonda si sahihi.
Askofu Gwajima: Taasisi nyingine za serikali kama DCI, Mawaziri, Polisi hawathubutu kuongea sababu ya "Makonda Syndrome."
Askofu Gwajima: Nimepigiwa simu na viongozi wengine wakinipa pole na mmoja wao aliyenitumia 'msg' ni Dkt Slaa.
Askofu Gwajima: Mamlaka aliyopewa Makonda ni makubwa na matumizi yake mabaya.
Post a Comment