DAR ES SALAAM: Saa kadhaa baada ya kuachiwa kwa dhamana kutoka Mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati (Centra) jijini Dar, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, amefanyiwa kisomo ili kumuondolea nuksi na kumuepusha na mabaya mengine yote yatakayotaka kujitokeza mbele yake.
Juzi (Alhamisi), Wema aliachiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar kwa dhamana ya shilingi milioni 5 baada ya kusomewa mashitaka matatu kukutwa na kiwango kidogo cha madawa ya kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08, iliahirishwa hadi Februari 22, mwaka huu itakaposikilizwa tena ambapo uchunguzi unaendelea.
MAMA WEMA AANDAA KISOMO
Habari za uhakika zilieleza kuwa, mara baada ya kutoka mahabusu, mama yake mzazi, Mariam Sepetu alifanya maandalizi ya kisomo maalum cha mwanaye huyo kwa kuwasiliana na mashehe mbalimbali ili kumuepusha mwanaye huyo na mabalaa. Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kuwa, kisomo hicho kilikuwa kinaendelea nyumbani kwa mama Wema, Sinza-Mori jijini Dar ambapo Risasi Jumamosi lilitinga eneo la tukio na kushiriki shughuli hiyo mwanzo hadi mwisho.
Kisomo hicho kiliongozwa na mashehe watano na wanafunzi wao walioonekana kuhuzunishwa na tukio hilo la Wema kuwekwa ndani kwa msala huo.
WEMA AZUNGUKWA
Kwa mujibu wa mashehe hao, Wema ambaye walimzunguka na kumfanyia kisomo hicho, atatakiwa kujiepusha na mambo yote yanayoweza kumletea mikosi ya aina yoyote na kwamba kutokana na kisomo hicho atakuwa ni mtu safi asiyekuwa na nuksi yoyote.
WASICHANA WAKE
Mbali na Wema, pia wasichana wake wawili akiwemo dada wa kazi ambao nao walikuwa mahabusu kisha wakaachiwa naye kwa msala huohuo, nao walifanyiwa kisomo hicho.
PETIT MAN NDANI
Wakati zoezi hilo likiendelea, pia alifika Petit Man ambaye naye alikuwa mahabusu kwa msala wa madawa ya kulevya kisha akafanyiwa kisomo kilichowahusisha pia ndugu wengine wa Wema. Baada ya kisomo hicho kilichodumu kwa takriban dakika arobaini, kilifuatiwa na chakula cha pamoja kilichoandaliwa nyumbani hapo ambapo watu walipata msosi na kutawanyika majira ya saa moja usiku.
Loading...
Post a Comment