Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MOVIE MPYA YA LULU 'FOOLISH AGE ' YAZINDULIWA KWA KISHINDO MLIMANI CITY JANA USIKU.... JIONEE MATUKIO YA AJABU YALIYOJILI UKUMBINI

 Elizabeth Michael Aka Lulu akitoa Shukrani kwaWadau wote waliojitokeza katika Usiku wake wa uzinduzi wa Filamu yake Mpya iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Proin Promotions Limited Geofrey Lukaza (Kushoto) akiwa na Waifu wake Groly Lukaza (katikakati) pamoja na Pedeshee Mamaa Ng'onzi wakijiachia Mbele ya Kamera ya Lukaza Blog usiku wa kuamkia Leo katika uzinduzi wa Filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited
 Lady Jay Dee aka Anaconda akitoa Burudani katika Uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited, Lady Jay Dee akiwa pamoja na Machozi Band walitoa Bururdani Safi Sana katika Uzinduzi huo Uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
Msanii Barnaba akitoa burudani katika uzinduzi wa Filamu mpya ya Lulu uliofanya na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
 Katikati ni Mama Mzazi wa Elizabeth Michael akiongea kwa furaha huku akitoa machozi na Msanii wa Filamu Tanzania Wema Abraham Sepetu(kushoto) na Rafiki yao katika Uzinduzi wa Filamu ya Lulu ulioandaliwa na kufanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Wema Sepetu (aliyepiga magoti) akikumbatiana na Mama yake mzazi Lulu wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Mwanae Elizabeth Michael katika Ukumbi wa Mlimani City, uzinduzi uliokwenda sambamba na burudani kutoka Kwa Wasanii mbalimbali wa Muziki wa Bongo Fleva katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo.
Wadau wakisakata Mduara katika uzinduzi huo wa filamu ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa kuamkia leo, Uzinduzi huo wa Kufa mtu uliofanywa na Kampuni ya Proin Promotions Limited ulifana kupita Kiasi
 Baadhi ya Wadau Mbalimbali waliojitokeza katika Uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Pron Promotions Limited.
Meza ya Viongozi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Kuanzia Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Bw Geofrey Lukaza, akifuatiwa na Pedeshee Mamaa Ng'onzi, Bwa Johnson Lukaza Mwenyekiti waa Makampuni ya Proin Tanzania, Gadna G Habash na Lady Jay Dee aka Anaconda wakiwa makini Kufuatilia Uzinduzi Mzima wa Filamu Mpya ya Lulu iitwayo Foolish Age uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited.

HUYU HAPA NDIYE ALIYEMJERUHI KWA CHUPA AUNT EZEKIEL

 

Just In: ... Rais Kagame, Museveni na Pierre Nkurunziza wazindua Bandari ya Mombasa

 
 
Marais wa Burundi, Uganda na Rwanda, wamehudhuria ufunguzi wa Bandari ya Mombasa, Kenya leo wakipokelewa wenyeji wao Rais Kenyatta na William Rutto!

Kenyatta anasema Mombasa ni 'Gateway of East African Business'. Anadai ni manifesto ya serikali yake kuifanya bandari hiyo kuwa 'busy and friendly port in all over East Africa coastline!'

Endelea kusoma zaidi => http://bit.ly/15gV9Aq
 
Marais wa Burundi, Uganda na Rwanda, wameudhuria ufunguzi wa bandari ya Mombasa, Kenya leo! Wapo pia na wenyeji wao President Kenyatta na Bwana Rutto!

Katika matangazo yao, wamesema bandari hiyo itaunganisha Africa kibiashara hasa ikichagizwa na Ujenzi wa barabara Namanga Arusha. Hii inaashiria nini kwa mustabali wa Uchumi wa Tz ambayo 60% ya makusanyo ya kodi yanategemea bandari ya Dsm!

Museveni kahudhuria kwa kiti chake cha Uenyekiti wa EAC, ndivyo Kagame alivyomtambulisha. Pia Kagame anasema hiyo ndio faida ya Integrated East Africa Community, pia Miundombinu bora ya Bandari ya Mombasa, itaunganisha nchi zote za East Africa.

Kenyata anasema Mombasa ni Gate way of East African Business. Anasema ni manifesto ya serikali yake kuifanya bandari ya Mombasa kuwa busy and friendly port in all over East Africa coastline!

Nini hatima ya bandari ya Dsm na siasa zake? Siasa za Kenya hizo wamezindua bandari mpya leo, na wanasema Sudan, Ethiopia na Somalia watatumia bandaria hiyo pia.

Live CITIZEN TV

Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi tisa akiwemo askari wa kituo cha polisi Oysterbay


Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limewatia mbaroni majambazi tisa wa kutumia siraha akiwemo askari polisi wa kituo cha Kipolisi oysterbay  jijin Dar es salaam.

Kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaamu  Bw.suleimani Kova amesema majambazi hao wamekamatwa katika operesheni maalum ya jeshi hilo ambapo pia walifanikiwa kukamata sare za jeshi la wananchi Tanzania(JWTZ) zinazoaminika kutumika katika uhalifu pamoja na silaha na risasi
Aidha kamanda kova ameeleza kukamata magari yanayosadikika kutumika katika uhalifu tofauti pamoja na yenye namba za usajili T865CEH aina ya carina,na T967 AUG carina.

Huyu ndio Mama aliyejifungua watoto wawili walioungana Dar, mmoja hana kichwa;

 

mama_56471.jpg
Mkazi wa Jang'ombe Visiwani Zanzibar, Pili Hija (24), amejifungua watoto walioungana huku mmoja akiwa hana kichwa.Watoto hao ambao wapo Wodi namba 36 katika Jengo la Wazazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili mbali na kuzaliwa mmoja akiwa hana kichwa, wameungana sehemu ya uti wa mgongo, mkono mmoja na wanatumia njia moja ya haja kubwa.
Akizungumza na mwandishi wetu jana, mama wa watoto hao, alisema: "Nilijifungulia nyumbani, nilisikia uchungu mara moja na hapo hapo nikajifungua kwa njia ya kawaida na jirani yangu ndiye aliyenisaidia,"alisema na kuongeza:
"Nilijifungua saa moja asubuhi, nilijua nitazaa pacha kwa kuwa nilishafanya kipimo katika Hospitali ya Makunduchi, wakaniambia nitajifungua pacha lakini mmoja si binadamu ni kiwiliwili.

Mtu 1 amefariki na 15 kujeruhiwa baada ya basi la Hood kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka

 Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali
Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .chanzo ITV

BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAWAKA MOTO ... WABUNGE WA TANZANIA WATOKA NJE YA UKUMBI


Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA)Magreth Zziwa akimsikiliza mbunge wa bunge hilo kutoka Tanzania,Shyrose Bhanji wakati wakielekea bungeni.

Spika akiongoza kikao cha leo mchana ambacho kiliahirishwa baada ya wabunge wa Tanzania kutoka nje

Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo kupinga wabunge wenzao wanaoshinikiza hoja zao kwa kutoka kwenye vikao vya bunge hali inayoshusha hadhi ya Spika,bunge na wabunge wenyewe,kutoka kushoto ni Mh.Twaha Taslima,Mh.Shyrose Bhanji,Mh.Abdula Mwinyi na Nderakindo Kessy

Mbunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari yalipo makao makuu wa Afrika Mashariki jijini Arusha baada ya kutoka nje na kikao kuhairishwa hadi kesho

POLISI MKOANI KATAVI YABAINI MTANDAO MPYA WA MATAPELI

 


SAM_2469Kibada wakibada, Katavi
POLISI  mkoani Katavi  imeubaini  mtandao  wa matapeli   uliojitanua katika  mkoani  humo  pia katika mikoa  ya Rukwa  na Mwanza  kwa  kuwatia nguvuni  vinara  wake akiwemo  mwanamke mmoja wakituhumiwa  kutapeli  watu  kwa kujifanya  wanatoa huduma  za uganga  wa jadi pasipo  kuwa  na  kibali .
Kamanda wa Polisi mkoani  hapa , Dhahiri Kidavashari  aliwataja   vinara  wa matandao  huo wa kitapeli  kuwa  ni pamoja na Issa Hassan(42) ,Hussein  Hassan  maarufu Rwango (38)  wakiwa wakazi wa jijiji la Mwanza,na Magreth Bakari (45)  mkazi  wa Mtaa wa Nsemlwa  mjini Mpanda  mkoani Katavi Charles  Mwelela (38.)akiwa ni mkazi wa sumbawanga mkoani Rukwa.
 Alibainisha hayo  leo  wakati  akizungumza na  waandishi  wa habari   ofisini  kwake  huku akiwaonesha  watuhumiwa hao  wanne  pia  tunguli  zao wanazodaiwa kuzitumia  kutapeli  wananchi mbalimbali  nchini ambapo  Agosti 26 mwaka  huu , saa  tano  usiku  watuhumiwa hao  walikamatwa  katika Mtaa wa Mji mwema mjini hapa  katika  nyumba ya kulala wageni  iitwayo Vatikani .
Miongoni  mwa  tunguli  hizo alizozioensha kwa  waandishi  wa  habari  na  baadhi ya  maofisa  wa  polisi  ni pamoja na ndege aliyekaushwa  ambaye  hutumika  kwa  kuwafanya  wanaume  watii  kila kitu  wanachoamriwa na wake  zao  ikiwemo  kupika  hadi  kufua nguo  za  wake  zao .

Makubwa Haya ... Wakazi wa Singida wadai dawa za Kichocho na Minyoo zinawaongezea nguvu za kiume.

 

MKUU
Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Dorothy Gwajima akitoa ufafanuzi wa masuala ya afya kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) waliomtembelea ofisini kwake.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Baadhi ya wananchi wanaomeza dawa za kutibu kichocho na minyoo ya tumbo kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini (NTD), wanadai zinawasaidia kuongeza nguvu za kiume wakati wa tendo la kujamiana.
Mratibu wa mpango huo mkoa wa Singida Yuda Machumu, amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya siku nne mjini Singida ya uandishi sahihi wa taarifa zinazohusiana na masuala ya afya.
Amesema kuwa baadhi ya wananchi hao wakishatumia dawa hizo hurudi tena kwa wagawa dawa wakihitaji kupatiwa tena dawa, kwa madai kwamba zinawasaidia sana kuwaongezea nguvu wakati wa kujamiana.

Ufafanuzi Kuhusu Wafadhili Kujitoa Kufadhili Shughuli Za Ukimwi Tanzania Kwanzia Mwaka Kesho 2014

 


 Tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) – Tanzania imepata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kwamba wahisani wa shughuli za UKIMWI kujitoa kufadhili shughuli za UKIMWI kuanzia mwaka kesho 2014.

TACAIDS, inafafanua kwamba tetesi hizo sio za kweli hata hivyo baadhi ya Wahisani ambao wanajitoa kwenye ufadhili kutokana na miradi wanayoifadhili kuisha muda wake au kubadilika vipaumbele kwa mfano Serikali ya Kanada na Denmark ambao wamekuwa wakisaidia Programu za UKIMWI kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na Jamii ambapo mradi wao unaisha 2016/17. Hata hivyo Serikali ya Denmark bado ina nia ya kuendelea kusaidia shughuli za UKIMWI, baada ya Mradi huo kuisha.


Utekelezaji wa shughuli za UKIMWI Tanzania umekuwa ukipata ufadhili wa fedha kutoka Serikali ya Tanzania na Serikali za Nchi Marafiki. Programu zinazotekelezwa hufuata Mkakati wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NMSF).Mpaka sasa kuna uhakika wa fedha za UKIMWI kwa miaka mitano (5) ijayo.

Maoni ya Baraza la Katiba la Wakuu wa Mikoa na Wilaya Yakabidhiwa Rasmi Kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba


 

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) maoni ya Baraza la Katiba la Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013). Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama na mwingine ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela.
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti. Mwingine ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 38, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto kwa Jaji Warioba), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti) na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela. Kushoto ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.

KATIBU MKUU JUMUIA YA WAZAZI AANZA KAZI KWA MIKWARA MIZITO



Seif Shabaan Mohamed
KATIBU Mkuu mpya wa Jumuia ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Seif Shabaan Mohamed  ameonya kuwa hatakuwa na huruma na kiongozi yeyote atakayefuja fedha za jumuia hiyo.
Alisema katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wake atahakikisha anafanyakazi kwa uadilifu na uamini mkubwa  na kwamba atakuwa mkali na makini kuhusu matumizi ya fedha za jumuia yake.
Mohamed alisema kila kiongozi anastahili kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, maadili na miiko kwa kutokana na dhamana aliyonayo na si vinginevyo.
Kauli Katibu Mkuu huyo mpya imekuja huku jumuia hiyo ikiwa imegumbikwa na wingu jeusi la matumizi mabaya ya fedha na hivyo kuifanya isue sue kwa kipindi kirefu badala ya kusonga mbele.
Aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Dodoma Hoteli wakati akiwashukuru Wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi kwa kumthibitisha kushika wadhifa huo.
Mohamed anashika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya aliyekuwa akiishikilia Khamis Suleiman Dadi kutoteuliwa tena na vikao vya juu vya CCM.
“Kwanza nashukuru kupata nafasi hii ya juu maana sikutegemea kama ingekuwa hivi, lakini niwaambie kwamba nitakuwa mkali sana na masuala fedha,” alisema Mohamed.

MAREKANI INAPOIZUNGUKA TANZANIA KUPITIA KWA RAIS KAGAME

                                                       

kagame_48210.jpgAliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton, hivi majuzi amemtetea Kagame kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuwasaidia waasi wa M23 nchini DRC.
Kwa muda wa miezi takriban minne kumekuwa na maneno ya kejeli kutoka kwa Serikali ya Rwanda na kwa hakika maneno hayo yanatoka mdomoni mwa Rais Paul Kagame na maofisa wa ngazi za juu katika Serikali yake.
Kagame amekuwa mbogo baada ya Rais Jakaya Kikwete kumshauri afanye mazungumzo na wapiganaji wa Kihutu waliokimbilia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) baada ya kutuhumiwa kufanya mauaji ya kimbari nchini mwake mwaka 1994.
Inakadiriwa kuwa Watutsi na Wahutu 800,000 wenye msimamo wa wastani waliuawa wakati huo, ingawa takwimu hizo zina utata, kwani wako wanaodai kuwa nchi hiyo wakati huo ilikuwa na idadi ndogo ya watu ambao idadi hiyo inasemekana ndio waliouawa.
Pia, wapo wale ambao wanaweza kushangaa kwa nini Kagame amekuwa hivyo na kuikosea heshima Tanzania, nchi ambayo imekuwa mstari wa mbele kupokea wakimbizi wake toka miaka ya 1960 na kwa nini Rais Kikwete alitoa ushauri huo.

WAZIRI LUKUVI AWAKAANGA WABUNGE SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA




DODOMA. 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amesema baadhi ya majina ya wabunge yametajwa miongoni mwa watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya lakini Serikali haiwezi kuwataja hadharani kwa haraka.
Majibu hayo ya Waziri Lukuvi yamekuja baada ya wabunge kumbana na wengine wakizomea baada ya kueleza ugumu wa kutaja majina ya washukiwa pasi na ushahidi wa kutosha.
“Serikali haiwezi kutaja majina haraka kiasi hicho kwani inaogopa kukurupuka na kushindwa mahak
amani, hivyo lazima tuwe makini sana na jambo hilo. Hatuwezi kukurupuka tu eti ni fulani wakati hatuna vithibitisho.
“Kumbukeni wengine mpo humu ndani ya Bunge na tukianza wengi mtakwisha maana katika orodha hiyo kubwa na ninyi mmo na orodha ni kubwa kweli ambayo wakati mwingine inatakiwa umakini wa hali ya juu,” alisema Lukuvi alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Karatu (Chadema), Mchungaji Israel Natse.

ABOUD AKUTA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA KUWAPA MAAGIZO MAZITO

               
  
01 2e7dc
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohd akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar juu ya suala zima la uboreshaji Sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Khadija Khamis na Amina Shaibu wa Habari Maelezo Zanzibar.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka viongozi wa vyama vya siasa kushirikiana na kutoa mchango wao wa hali na mali katika kufanikisha sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Abuod Muhammed alipokutana na wawakilishi wa vyama vya siasa ofisini kwa ke Vuga.
Alisema kuwa Serikali imeamua kuzifanya sherehe hizo kuwa za aina yake na zinahitaji mchango wa kila mtu bila ya kuangalia itikadi ya vyama vya siasa ili kuonyesha uelewa wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini.

YANGA, COASTAL UNION WAGAWANA POINTI;SIMBA, AZAM FC ZAZOA POINTI UGENINI

MABINGWA wa ligi kuu bara, Yanga Sc leo wamegawana pointi  na 'Wagosi wa Kaya' Coastal Union ya Tanga na kujikuta wakitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Aidha, Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc na Wanalamba lamba Azam Fc waliokuwa wakicheza ugenini wamefanikiwa kuondoka na pointi tatu muhimu.
Katika mchezo wa Yanga na Coastal ambao ulitawaliwa na rafu za hapa na pale baina ya wachezaji,timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadilikmo ambapo nyota wa kimataifa wa Yanga Didier Kavumbagu, huku timu hizo zikicheza pungufu baada ya wachezaji wake kutolewa kwa kadi nyekundu.
Zikiwa zimebaki dakika chache kabla ya mwamuzi Martin Sanya kupuliza kipenga cha kumaliza mchezo, Jerry Santo aliisawazishia Coastal kwa penalti.
Nao Simba Sc  leo imeondoka na poinbti tatu muhimu baada ya kuwatandika maafande wa JKT Oljoro kwa bao 1-0, a mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na mfungaji akiwa ni Haruna Chanongo.
Kwa upande wa Azam Fc nao wameweka kibindoni pointi tatu baada ya kuwatandika Rhino ya Tabora mabao 2-0 kattika mchezo ulifanyika uwanja wa Ally hassan Mwinyi na mabao ya Azam yalipachikwa na Gaudance Mwaikimba na Seif Karihe.
Michezo mingine ya ligi hiyo leo ilikuwa ni kama ifuatavyo
MBEYA CITY  V  RUVU SHOOTING 2-1
MGAMBO SHOOTING  v  ASHANTI UNITED 1-0
MTIBWA SUGAR  V  KAGERA SUGAR  1-0
JKT RUVU v TZ PRISONS 3-o

TPSF: Serikali isitishe ugawaji wa vitalu vya gesi



 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. (Picha na Francis Dande) 
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF, Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera ya uwekezaji nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte. 

'RADIO IMAAN FM NA NEEMA FM ZATOKA KIFUNGONI'



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
                                                                                               
                                                                                        KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO
1.0 Utangulizi:
Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.
Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-
a)   Vituo vyote vilipewa  onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;
b)  Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.
2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo
      na Mamlaka ya Mawasiliano:   

Grand Malt yamwaga vifaa Ligi Kuu Z’bar



Mwakilishi wa timu ya KMKM ya unguja  Said Mfaume akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Mwakilishi wa timu ya Mafunzo  ya pemba  Khamis Ally akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA, Ravia Faina. 
Mwakilishi wa timu ya jamhuri  ya pemba  Abdallah Abeid  akipokea jezi toka kwa Waziri wa habari,utalii na michezo Zanzibar Said Mbarouk tayari kabisa kwa kuanza kwa ligi kuu ya Grandmalt Zanzibar,Kulia ni meneja masoko wa GrandMalt Fimbo buttala na Rais wa ZFA Ravia Faina.

CAG ATUMWA KUCHUNGUZA TUHUMA DHIDI YA MEYA WA BUKOBA ANATORY AMANI



RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA MEYA WA BUKOBA DK ANATORY AMANI HIVI KARIBUNI. 

DODOMA. 
KAMATI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC-CCM) kimeiomba Serikali kumtuma Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kwenda Bukoba, Kagera kuchunguza tuhuma dhidi ya Meya wa Manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kamati hiyo imew
aagiza Mbunge wa Bukoba Mjini, Khamis Kagasheki na Dk Aman kurudisha utulivu wa kisiasa katika Manispaa hiyo ambayo katika siku za karibuni imekuwa na mgogoro mkubwa.

MBEYA CITY YAITANDIKA RUVU SHOOTING BAO 2--1

 


Mgeni rasmi meya wa jiji laMbeya Athanas Kapunga  akisalimiana na wachezaji wa Mbeya city kabla ya mechi kuanza

Meya wa jiji la Mbeya akiongea na timu zote mbili


Wachezaji wa timu ya Mbeya city wakishangilia ushindi baadya ya kuitandika Ruvu shooting

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA WATENDAJI WA KAMATI YA MJI MPYA WA MABWE PANDE

 


 Msaidizi wa Makamu wa Rais wa masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akimkabidhi Pikipiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, aliyeikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande, Abdallah Kunja.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, akimkabidhi Pikipiki na nyaraka muhimu, Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande, Abdallah Kunja, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo mpya, ambapo Mkuu wa Wilaya, alikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais.

Ziara ya Rais Dr. Shein nchini Uholanzi

 


IMG_2462
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam,Rene Van Der Plas,alipotembelea katika bandari hiyo  akiwa katika Ziara ya siku tano na ujumbe wake, nchini Uholanzi, {Picha na Ramadhan Othman Uholanzi]. IMG_2496 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,alipokuwa akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,ukioongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ziara nchini Uholanzi.  [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.] IMG_2524
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Mitambo ya usambazji wa Gesi inayotumika katika nchi za ulaya,(GATE TERMINAL) Dick Meurs,walipofika katika Ofisi za Kituo hicho huko katika Bandari ya Rotterdam,nchini Uholanzi katika ziara ya siku tano. [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.] IMG_2542
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)na Mawaziri pamoja na Balozi Dr.Diadorus B. Kamala,(wa pili kulia)wakizungumza na Makamo wa Rais pia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari ya Rotterdam, Rene Van Der Plas,walipokuwa katika Boti walipoitembelea Bandari ya Rotterdam Nchni Uholanzi wakiwa katika ziara ya siku tano nchini humo.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top